Saturday, August 08, 2015

UTT-PID YASHIRIKI MAONYESHO YA NANE NANE – LINDI


Maafisa Masoko wa UTT-PID, Bi Kilave Atenaka (katikati) na  Bi. Mary Minja (kwanza kulia) wakiongea na mteja aliyefika banda lao lililo chini ya wizara ya Fedha katika Maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Afisa Masoko UTT-PID, Bi Kilave Atenaka akihudumia mteja katika banda lao lililo chini ya wizara ya Fedha katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Afisa Masoko UTT-PID, Bi Kilave Atenaka akihudumia mteja katika banda lao lililo chini ya wizara ya Fedha katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Muonekano wa viwanja vya Mabano vilivyopimwa na Taasisi ya UTT-PID kwa ushirikiano na Halmashauri vilivyopo Manispaa ya Lindi.
Zaidi ya viwanja 2,500 vilipimwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile Makazi, Biashara, Maeneo ya Umma na sehemu za kupumzika.  
 Akielezea Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka alisema kuwa kwa sasa wanaendesha huduma ya uuzwaji wa Fomu kwa ajili ya Viwanja, pia wanatarajia kuanza kuuza kwa umaa na taasisi mbali mbali miradi mipya ikiwemo wa Tundwi Songai – Kigamboni jijini Dar es Salaam na ule wa Kingorwila, Morogoro.

Aidha Bi. Kilave alitumia wito huo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ndani ya banda hilo kujipatia elimu mbali mbali zitolewazo na taasisi hiyo hapa nchini.

Toka kuanzishwa kwake Taasisi ya UTT-PID imejikita sana katika upimaji wa maeneno katika mikoa mbalimbali kwa kushirikiana na Halmashauri tofauti nchini. Miradi mikubwa kama ya Bukoba ambapo viwanja zaidi ya 5,000 vilipima kuuzwa, Halmashauri ya Sengerema kwa ushirikiano na Taasisi ilipima zaidi ya viwanja 1,200 na uuzaji pamoja na uwekezaji katika Miundombinu husika unaendelea kwa kasi. Pia Taasisi imewekeza katika miradi binafsi kama vile eneo la Mapinga katika wilaya ya Bagamoyo huku ikatarajia uwekezaji mkubwa zaidi katika mikoa ya Morogoro , Arusha, Dar es Salaam, Maswa, Pwani, Maswa na Ruvuma.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...