Wednesday, June 17, 2015

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA LINDI KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi ameanza ziara Mkoani Lindi ili kukagua shughuli za Shirika la Nyumba la Taifa na kusikiliza migogoro ya ardhi kwa nia ya kuitatua. Katika ziara hiyo, Waziri Lukuvi ameiagiza NHC kuandaa orodha ya wadaiwa sugu wa taasisi, idara na Wizra za Serikali ili iwasilishwe kwake aweze kuipeleka Hazina ili madeni hayo yakatwe moja kwa moja. Aidha, ameitaka NHC kuitumia vema ardhi inayoimiliki eneo la Mitwero katika Manispaa ya Lindi kwa kujenga nyumba zitakazokuwa na hadhi kwa miaka kumi ijayo kwa kuwa mji wa Lindi na Mtwara unakua kwa kasi.
11
Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi Bw. Mussa Patrick Kamendu akimpokea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi mara baada ya kuwasili Mkoani humo kuanza ziara ya siku mbili.
1
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akisalimiana na watendaji wa NHC mara baada ya kuwasili Mkoani humo kuanza ziara ya siku mbili.
3
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Mwantumu Mahiza akitoa taarifa fupi ya Mkoa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi mara baada ya kuwasili Mkoani humo kuanza ziara ya siku mbili kutatua migogoro ya Ardhi. Mh. Mahiza alielezea ushirikiano uliopo kati ya Mkoa na NHC wa kuwezesha ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Mkoa huo.
4
Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi Bw. Mussa Patrick Kamendu akitoa taarifa ya Mkoa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi mara baada ya kuwasili Mkoani humo kuanza ziara ya siku mbili kutatua migogoro ya Ardhi.
5
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akikagua matengenezo ya nyumba ya NHC iliko kiwanja namba 23 na 25 Mtaa wa Herieth Mjini Lindi.
6
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akikagua matengenezo ya nyumba ya NHC iliko kiwanja namba 23 na 25 Mtaa wa Herieth Mjini Lindi.
7
Matengenezo ya ukumbi mkubwa kuliko kumbi zote za starehe zilizopo Mtwara na Lindi unaomilikiwa na NHC katika Manispaa ya Lindi ulikaguliwa na Waziri Lukuvi na kupongeza kiwango cha matengenezo kilichofanyika.
8
Nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mtanda katika Manispaa ya Lindi zinavyoonekana baada ya kukamilika ujenzi wake na kuuzwa kwa wananchi wa Manispaa hiyo.
9
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mtanda katika Manispaa ya Lindi.
10
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akikagua viwanja vinavyomilikiwa na NHC eneo la Mitwero lililoko kilomita kumi kutoka Manispaa ya Lindi.
2
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akitoa maelekezo kwa watendaji wa NHC ya matumizi sahihi ya ardhi inayomilikiwa na NHC eneo la Mitwero Manispaa ya Lindi ambapo alitaka nyumba zitakazojengwa katika eneo hilo zibebe thamani ya ardhi kwa miaka kumi ijayo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...