Na Salma Ngwilizi – Maelezo
………………………………
Benki ya Tanzania(BOT) imewataadharisha wananchi kwamba sarafu ya sh. 500 haina madini ya aina yoyote na wala haiuzwi kama inadaiwa baadhi ya watu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Zalia Mbeo wakati akitoa ufafanuzi kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mwizu ambaye aliuliza kwamba kuna taarifa kuhusu sarafu hiyo kuuzwa mitaani .
Kaimu Katibu Mkuu huyo ambaye alifungua maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani.
“Watanzania wanatapeliwa sarafu hii haina thamani yoyote ni uzushi,” alisema Zalia.
Aliongeza wananchi wadanganywa na watu kuwa sarafu hiyo ikiyeyushwa ina madini ambayo yanaweza kuwapatia fedha nyingi wakati si kweli.
Maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yamefunguliwa rasmi leo Juni 16, mwaka huu na yanatarajia kumalizika Juni 23, mwaka huu.
Kauli mbiu ya mwaka huu “Utumishi wa Umma katika Bara la Afrika ni chachu ya kuwawezesha Wanawake kuongeza Ubunifu na Kuboresha utoaji wa Huduma kwa Umma”.
No comments:
Post a Comment