Sunday, June 28, 2015

MAFURIKO YA LOWASSA YAHAMIA JIJINI DAR, AKOMBA UDHAMINI WA WANACCM 212, 150

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akifurahia jambo wakati Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Ramadhan Madabida (hayupo pichani) akizungumza jambo, wakati Mh. Lowassa alipofika ofisi ya CCM Mkoa huo, Mtaa wa Lumumba.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Ramadhan Madabida akizungumza jambo kumuhusu, Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (kulia), wakati alipofika kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam kusaini kitabu, wakati akiwa katika ziara yake ya kutafuta saini za WanaCCM wakumdhamini ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 212, 150 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi ya WanaCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakimshangia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Ramadhan Madabida (hayupo pichani) .
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, Mkewe Mama Regina Lowassa pamoja na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu wakiwa sambamba na wanaCCM wengine wakati wakiwasili kwenye Ofisi za CCM Tawi la Ilala Kota, Mchikichini jijini Dar.

Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Ernest Chale akikabidhi fomu za Wadhamini kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa. Jumla ya WanaCCM 44,299 wa Wilaya ya Ilala Wamemdhamini Mh. Lowassa ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.

Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu akiwasalimia wananchi wake.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akiwasalimia wanaCCM wa Wilaya ya Ilala, Jijini Dar.





Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia WanaCCM wa Wilaya ya Ilala, waliokusanyika kwa wingi kwenye Uwanja wa CCM Tawi la Kota, Mchikichini Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Assah Simba akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa kuwasalimia na kuwashukuru wanaCCM wa Wilaya ya Ilala waliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika .
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na kuwashukuru wanaCCM wa Wilaya ya Ilala waliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2015.
Sehemu ya Vijana wa CCM wakifatilia kwa makini salam za Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya kinamama wenye ulemavu wa Miguu waliokuwepo kwenye hadhara hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na kinamama wa CCM Wilaya ya Ilala.
Umati wa Watu ukiwa umejipanga barabarani kumuona Mh. Lowassa akipita kuelekewa Ofisi ya CCM Wilaya ya Temeke, Jijini Dar .
MwanaCCM Wilaya ya Temeke akisini fomu ya Udhamini mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa.
Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke, Robert Kerenge akikabidhi fomu za Wadhamini kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa . Jumla ya WanaCCM 72, 100 wa Wilaya ya Temeke Wamemdhamini Mh. Lowassa ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akisalimia wananchi wake.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na kuwashukuru wanaCCM wa Wilaya ya Temeke kwa kumdhamini ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Jiji la Dar ilikuwa ni shangwe tupu kwa kila alieweza kumuona Mh. Lowassa akipita kwenye njia zilizo jirani na maeneo yao ya kazi.
Dereva akipuliza tarumbeta kuonyesha furaha yake kwa Mh. Lowassa.
Mh. Lowassa akiwasili kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni, Mkajuni jijini Dar.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Mtoto Shadrack Samuel (5) alitaka kumsalimia na kumuona. 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru . 
Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan akisalimia wananchi wake.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Dodoma akiwasalimia wanaCCM wa Kinondoni jijini Dar.
Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akizungumza machache na WanaCCM wa Wilaya ya Kinondoni, Waliomdhamini Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa. ambapo kwa wilaya ya Kinondoni amepata udhamini wa wanaCCM 95, 251 na kufanya jumla kuu kuwa 212, 150 na kuifanya Dar es salaam kuwa Mkoa wa kwanza kuwa na idadi kubwa ya WanaCCM waliomdhamini Mh. Lowassa.
Wadau Mkutanoni.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...