Friday, June 19, 2015

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA INDRA GANDHI NA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MATREKTA CHA NEW HOLLAND TIAT HUKO NEW DELHI.

01
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongozana na Mke wa Balozi wa India nchini Tanzania Mheshimiwa Debnath Shaw wakielekea kwenye jengo la Makumbusho ya Indra Gandhi huko New Delhi tarehe 18.6.2015. Mama Salma yupo nchini India akiambatana na Rais Kikwete kwenye ziara siku 4 ya kiserikali  kwa mwaliko wa serikali ya India.
03
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea sehemu mbalimbali zilizohifadhiwa kumbukumbu za aliyekuwa Waziri Mkuu wa India Marehemo Indra Gandhi wakati wa uhai wake. Marehemu Idra Gandhi aliuawa kwa kupigwa risasi tarehe 31.10.1984 akiwa kwenye viwanja vya nyumba hiyo ambayo alikuwa
07
04
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya Marehemu Indra Gandhi wakati alipotembelea makumbusho ya waziri mkuu huyo huko New De;lhi nchini India tarehe 18.6.2015.
05
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na kiongozi anayesimamia Makumbusho ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa India Marehemu Indra Gandhi (jina lake halikuweza kupatikana) mara baada ya kumaliza kutembelea makumbusho hayo tarehe 18.6.2015.
06
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  akipewa taarifa mbalimbali na Bwana  Rajan Madan, Mkurugenzi wa Uzalishaji  katika Kiwanda cha New Holland Fiat Limited kuhusiana na utengenezaji wa matrekta kwenye Kiwanda hicho  huko New Delhi. Mama Salma Kikwete aliambatana na Rais Kikwete kuzuru kiwandani hapo ili kujionea utengenezaji wa matrekta.
 PICHA NA JOHN LUKUWI.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...