Waziri William Vangimembe Lukuvi akisisitiza jambo baada ya Watendaji wa sekta ya ardhi ya Mkoa wa Lindi kushindwa kumudu maswali mbalimbali aliyowauliza na kuwataka watendaji hao kujipima kama bado wanastahili kuendelea kuwatumikia wananchi kwa nafasi zao wanazotumimkia.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Mwantumu Mahiza akimuomba Mheshimiwa William Lukuvi kuwaondoa watendaji wabovu wa sekta ya ardhi Mkoani Lindi akisema kuwa wapo watanzania wengi wenye uwezo wa kufanya kazi zao. Alisema kuwa hayuko tayari kuyumbisha kiti chake alichoaminiwa na Rais kwa kuwalea watendaji wazembe.
Sehemu ya umati wa wananchi waliofika eneo la Mitwero kuwasilisha kero zao kwa Waziri William Lukuvi. Malalamiko mengi ya wananchi yanatokana na kutokushirikishwa katika uthamini wa ardhi na mali yao hali ambayo imewafanya kupunjwa malipo ya fidia. Waziri Lukuvi ameagiza wanaothamini mali ya wananchi kote nchini kufanya kazi hiyo kwa uaminifu na kuwashirikisha wananchi hao katika hatua zote ili kuondoa malalamiko na kutenda haki.
Waziri Lukuvi akimhoji Mpima ardhi wa MANISPAA YA Lindi Bw. Mpoki baada ya kulalamikiwa na wananchi wengi kuwa anatabia ya kuomba rushwa ili kuwapa huduma wananchi. Waziri Lukuvi ameapa kutomsamehe Afisa yeyote wa sekta ya Ardhi atakayetajwa na wananchi na kubainika kula rushwa na kwamba uchambuzi wa malalamiko ya wananchi ukikamilika ataanza kuchukua hatua za kinidhamu kwa watendaji wabovu na wala rushwa.
Mwananchi aliyebahatika kutoa dukuduku zake kwa Waziri Lukuvi akimuonyesha Afisa anayelalamikiwa kwa rushwa katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi eneo la Mitwero lililopo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Mwantumu Mahiza atiktoa taarifa ya migogoro ya Ardhi ya Mkoa wa Lindi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi alipowasili Ofisini kwake.
Sehemu ya Watendaji wa Mkoa wa Lindi wakiwemo Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wakimsikiliza Waziri Lukuvi(hayupo pichani) alipozungumza nao katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kusisitiza uadilifu katika sekta ya ardhi ili kuhudumia wananchi kwa haki na kuondoa kero za ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akiongea jambo na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa LindI tayari kuanza kikao cha Watendaji wote wa Mkoa huo.
Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akishangazwa na uamuzi wa Manispaa ya Lindi wa kupimiwa ardhi na UTT kwa gharama kubwa jambo ambalo wangelifanya wao ili kujenga uzoefu, kupata faida kubwa na kupunguza gharama ya kupima na hatimaye kuuza viwanja hivyo kwa wananchi. Ameagiza kupitiwa upya makubaliano waliyofanya na UTT ili kupata fedha za kuwaongeza fidia wananchi wanaolalamikia kupunjwa fidia eneo la Mitwero, nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.
Wananchi kadhaa wakimpongeza Waziri Lukuvi kwa kuweza kutatua migogoro yao ya ardhi iliyodumu kwa miongo miwili na zaidi alipomaliza mkutano wa kuwasikiliza na kuagiza mambo mbalimbali ya kuondoa kero za wananchi.
No comments:
Post a Comment