Thursday, June 25, 2015

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, LAZARO NYALANDU APATA WADHAMINI MKOANI RUVUMA

2
 WANACHAMA na mashabiki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Ruvuma, wakishangilia kwa furaha wakati Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akiwasili kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Ruvuma, kuomba udhamini katika harakati zake za kuwania kuteuliwa kuwania urais kupitia CCM.
3
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akizungumza na wanachama wa CCM waliojitokeza kumdhamini katika harakati zake za kuwania kuteuliwa na Chama kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.
4
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akikabidhiwa fomu za udhamini na Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Verena Shumbusho, baada ya kudhaminiwa na zaidi ya wanachama 90.
5
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akipokewa na mamia ya wanachama, mashabiki na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alipowasili mkoani Ruvuma jana, kuomba udhamini katika harakati zake za kuwania kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya urais.
689

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...