Tuesday, June 30, 2015

KINANA ZIARANI UKEREWE

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia wakazi wa kijiji cha Sambi kata ya Irugwa, wilayani Ukerewe waliojitokeza kwa wingi kumpokea ,Kinana ameweka historia kwa kuwa kiongozi wa kwanza kufika katika kisiwa hicho akiwa kwenye ziara ya kukagua, kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi pamoja na kukagua uhai wa Chama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimina na mmoja wa wakazi wa kata ya Irugwa
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Sambi kata ya Irugwa.
 Wananchi wa Kata ya Irugwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiwapingia mkono wananchi waliojitokeza kumpokea kwenye kisiwa cha Ukara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifuturu ndani ya meli ya Mv.Nyerere akiwa njiani kuelekea Nansio Ukerewe, Wengine pichani ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Mhe. Antony Diallo (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Magessa Mulongo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa Nansio waliojitokeza kwa wingi kumpokea.
(Picha na Adam Mzee)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...