Monday, June 22, 2015

WANAKIJIJI ITUNDU KATA YA MLANGALI WATAKA FILIKUNJOMBE KUENDELEA UBUNGE WAMCHANGIA TSH 65,200 ZA FOMU

Mwanamke  mkazi   wa kijiji  cha Itundu kata ya  Mlangali  wilaya ya  Ludewa akimchangia  mbunge  wa  jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe wa pili  kushoto pesa ya fomu ya  ubunge wa kwanza kushoto ni katibu wake Bw Stany Gowele
Wananchi  wakimchangia mbunge  Filikunjombe pesa za kuchukua fomu ya ubunge
Mbunge Filikunjombe  akichangiwa  pesa  ya  kuchukulia  fomu ya  ubunge muda ukifika
Mbunge  Filikunjombe akifurahia  kuchangia pesa  ya kuchukulia  fomu ya ubunge
Wananchi wa kada mbali mbali  wakimchangia mbunge Filikunjombe
Filikunjombe akikabidhi sare  kwa madereva  boda  boda Mlangali
Kwaya  ya  vijana  wakiimba  wimbo  wa  kulinda amani  wakati wa mkutano wa mbunge Filikunjombe.
Mbunge  Filikunjombe  akizungumza na  wananchi  wa kijiji  cha Itundu kata ya Mlangali Ludewa.
Filikunjombe akitoa  mfano  wa mshikamano  wa  kimaendeleo  unavyoweza  kuleta mabadiliko makubwa.
Mbunge  wa Ludewa Deo  Filikunjombe  akikabidhi   vifaa vya  michezo kwa timu zote 8 za  vitongoji  vya kijiji cha Itundu  kata ya Mlangali

Na matukiodaimaBlog,Ludewa
WANACHAMA  waasasi  za
fedha   vijijini kutoka   vikundi zaidi ya saba  vya Vicoba na
Sliki pamoja na  wananchi  wa kijiji
cha Itundu kata ya  Mlangali  wilaya
ya  Kilolo mkoani Njombe  wamemchangia
mbunge wa  jimbo la  Ludewa
Bw  Deo Filikunjombe kiasi cha Tsh
65,200 kwa  ajili ya  kuchangia fedha  za
kuchukua  fomu ya  kuwania ubunge kwa muhula wa  pili katika
jimbo  hilo la Ludewa.
Pamoja na kuchangia   pesa  hiyo
pia   wakazi wa kata   hiyo
kupitia   wazee  wa kijiji
cha  Itundu  walikitaka
chama  cha  Mapinduzi (CCM) kutoruhusu wana CCM
wengine  kuchukua fomu ya ubunge
katika   jimbo la Ludewa ili wao  kuweza
kuendelea na  mbunge  wao
wa  sasa  kutokana na
utendaji kazi  wake kiasi cha  kuwakomboa
wananchi  wa Ludewa . 
Wananchi  hao  waliyasema
hayo  jana   kwa nyakati
tofauti wakati  wa   hafla
ya uziduzi wa vikundi hivyo  na
mkutano  wa hadhara  uliofanyika katika  viwanja wa Stendi katika kijiji
hicho cha Itundu .
Mzee  Augustino
Msemakweli  na mzee Herbert Kayombo   walisema
kuwa  ni  mbunge
wa kwanza kwa  jimbo hilo la  Ludewa
kati ya  wabunge  zaidi ya 6
waliopata  kuongoza kufanikisha  utekelezaji
wa ahadi zake kwa  wakati na  kuwa wao kama 
wazee wa kijiji  hicho na  ni miongoni mwa  wazee wa jimbo la Ludewa ambao ni makada wa
CCM kilio chao  kwa  sasa ni kuona mbunge  huyo anaendelea kuongoza jimbo  hilo zaidi
pamoja na kuwasaidia kuwapigania
wazee  ili kuweza  kuliptwa mafao  ya uzeeni kutoka  serikalini.
Mzee  Msemakweli  alisema
kuwa  amepata  kusoma moja kati ya gazeti la wiki  kutoka Zanzibar  na
kuonyesha ni kiasi gani serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar
ilivyoweka mkakati  wa
kuwasaidia  wazee  kwa
kupanga  kumlipa mafao mzee  kila mwezi
kiasi cha kuanzia Tsh 20,000 hivyo
kuomba mbunge  wao kuendelea  kuungana
na  wabunge wengine  ili nao
waweze kulipwa mafao ya uzeeni.
Wakati   mzee
Kayombo  akieleza kufurahishwa na
utendaji wa Filikunjombe na  kusikitishwa
na mbinu  chafu za upinzani katika
kata   hiyo  inayoongozwa na diwani  wa chadema na mwenyekiti wa Chadema kuwazuia wananchi kulima katika
mabonde ( Vinyungu)na  kuwa  wanafanya
hivyo  kwa  lengo la
kukwamisha jitihada za  mbunge
wao.
Kwani  alisema  katika
kijiji  hicho wananchi miaka  yote
walikuwa  wakilima kwenye  vinyungu
kutokana na  eneo hilo  kutokuwa na chanzo  cha maji na
hata  umeme  wanaotegemea 
kupata  hauzalishwi katika  kijiji
hicho  .
Alisema  kuwa serikali
ya  kijiji  inawataka
wananchi  kutolima umbali  wa mita 60 ya
mto  wakati umbali  huo ni mkubwa
ukilinganisha na ukubwa wa
eneo   hilo.
Kuhusu mtazamo
wa  wananchi  wa
Ludewa juu ya utendaji kazi wa mbunge
huyo alisema  wao kama  wazee wamefurahishwa na kazi zinazofanywa na mbunge  huyo na
kuwa wao kama  wapiga kura
wanahitaji mtu na  sio  chama na kama chama kitaona Filikunjombe
hawafai  wao kama  wananchi hawatakuwa tayari kuunga mkono
maamuzi  yoyote  nje ya matakwa  yao.
Hata   hivyo  alisema
kuwa changamoto  kubwa ya  kijiji
chao kwa sasa ni maji na umeme na kumshukuru mbunge kwa kuwasaidia
gari la  wagonjwa katika  kijiji na kata yao  ya Mlangali .
Kwa  upande wake Emmanuel
Mpogole akizungumza kwa niaba ya wanachama
wa vikundi  vya kifedha  vijijini alisema  kuwa kumekuwepo na hamasa  kubwa ya uanzishwaji  wa
vikundi  hivyo toka  alipoingia mbunge  huyo madarakani na kuwa hali ya  uchumi wao
imezidi  kuboresheka  zaidi.
Akizungumza na
wananchi hao  mbali  ya kuwashukuru kwa mchango wao wa  fedha za
kuchukulia fomu Bw  Filikunjombe
alisema kuwa  imani ambayo  wananchi
wanaionyesha kwake ni  kubwa na
kuwa mbali ya  kutumia kiasi cha Tsh  milioni 75 kwa wilaya  nzima kila mwaka  kusomesha
watoto zaidi ya 20  kila kata  bado kata
hiyo ya Mlangali  ndio kata  pekee ambayo
mmoja kati ya  wanafunzi
aliowasomesha  alifika kushukuru na   hivyo kwa mwaka   mwakani kata
hiyo atasomesha  watoto 30 badala
ya 25 kama kata  nyingine.
Pia  alisema suala la
maji bado  wa kulaumiwa ni  viongozi wao wa  kijiji ambao hata katika taarifa ya kijiji
kwa mbunge hawaonyeshi kama  wana tatizo
la maji kama  viongozi wa vijijini  vingine ambao taarifa  zao
hueleza  wazi changamoto mbali
mbali .
Bw  Filikunjombe  alisema mbali ya viongozi wao kutoeleza
tatizo hilo la maji ila kwa upande wake analichukua  ili
kuanza kushughulikia kumaliza
kero ya maji katika  kijiji  hicho .
Mbunge  huyo
katika  kuunga mkono  vikundi vya
kifedha  vijijini aliahidi  kusaidia
kutoa mafunzo  ya ujasliamali
kwa  wanachama  wote
wa vikundi  zaidi ya 7 vya  kifedha
vijijini pamoja na  kila  kikundi kukichangia kiasi cha Tsh 500,000
huku  kikundi  cha boda boda akikichangia kiasi cha Tsh
milioni 2.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...