Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (Tanapa),Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari kwenye Makao makuu ya shirika hilo leo jijini Arusha juu ya utoaji Tuzo za umahiri wa uandishi wa habari za Utalii na Uhifadhi utakaoaofanyika Jumatatu ,Juni 28,2015 jijini Mwanza.
Waandishi wa habari kutoka taasisi mbalimbali jijini Arusha wakiondoka Makao Makuu ya Tanapa baada ya kumaliza mkutano huo.
………………………………………………………………………….
Na Filbert Rweyemamu,Arusha
Shirika la Hifadhi za Taifa nchini(Tanapa)litatoa Tuzo za umahiri wa Uandishi bora wa Habari na Makala zinazohusu Utalii na Uhifadhi nchini kwa waandishi wa Habari nchini ikiwa ni kutambua mchango wako katika kukuza sekta hiyo nchini.
Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Arusha,amesema maandalizi yote yamekamilika na utoaji Tuzo utafanyika jijini Mwanza,Jumatatu,Juni 28,mwaka huu.
Amesema idadi ya washiriki imekua ikiongeza kila mwaka hasa waandishi wa kutoka nje ya miji mikubwa kama Dar es Salaam,Arusha na Mwanza hali inayoonyesha mashindano haya kukua.
“Tumeshuhudia mwaka huu waandishi wengi kutoka mikoa ambayo awali haikushiriki lakini wakati huu wapo waandishi wa Redi za kijamii ambao kazi tumezipokea,”
Washindi wanatarajiwa kujipatia fedha taslimu na kupata safari za mafunzo katika moja ya nchi za Sadc.
Shelutete amesema kwa kipindi cha miaka minne washindani wamekua wakichaguliwa kutoka vyombo vya habari vya Runinga(TV)Radio na Magazeti lakini mwaka ujao wigo utapanuliwa na kujumuisha Mitandao ya Kijamii na Wapigapicha.
No comments:
Post a Comment