Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Hamis Kagasheki (katikati)akiwa na viongozi wa Chadema ,Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ,Freeman Mbowe akiteta jambo na Mkurugenzi wa Hali Halisi Publisher wachapishaji wa Mawio na Mwanahalisi Online,Sued Kubenea wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akipeana mkono Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ,Freeman Mbowe wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chadema ,Dk Wilbroad Slaa akiteta jambo na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waombolezaji wa kuaga mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akitoa hishima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chadema ,Dk Wilbroad Slaa akitoa hishima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima na Sayari wakiwa katika huzuni wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Safari ya kuelekea Kagera kwaajili ya maziko ya Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.)
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.
MAMIA wamejitokeza katika kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Mawio na Mwanahalisi online ,Edson Kamukara aliyefariki mwishoni wiki na anatarajiwa kuzikwa Juni 29 mkoani Kagera.
Wakizungumza wakati wa kuaga kwa aliyekuwa Mhariri wa Mawio na Mwanahalisi online ,Edson Kamukara wamesema ni pigo kwa tasnia ya habari kutokana na kuwa na kusimamia kitu anachoamini kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari .
Akizungumza juu ya kifo chake ,Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema kifo cha kamukara ni pigo kutokana na kuwa na msimamo wa bila kuyumbusha na bahasha.
“ Ni bora kuishi kwa kusimama kwa muda mrefu kuliko kuishi kwa kupiga magoti kwa muda mfupi hiyo ikiwa ni kuangalia kutumia kalamu kwa wanyonge bila masilahi ya wanasiasa”amesema Mbow.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP.Reginard Mengi amesema Kamukara alikuwa jasiri katika kufanya mbambo yake kwa kusimamia misingi ya habari na alikuwa hangalii fedha.
“Fedha angekuwa Kamukara anaiangalia basi angekuwa tajiri kwani alikuwa ni mtu kusimamia misingi ya habari kwa ajili ya wanyonge”amesema Mengi.
No comments:
Post a Comment