Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za wanachama 33,780 wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, waliomdhani ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini, Loth Ole Nesele.
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro jana Juni 18, 2015, wakati shukrani kwa udhamini wa kishindo alioupata kutoka wa WanaCCM hao, ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 33,780.
Umati wa wanaCCM wa Mkoa wa Kilimanjaro, ukimshangilia kwa furaha, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati alipopanda jukwaani kuwashukuru wa kumdhamini kwa kishindo. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 33,780.
Sehemu ya WanaCCM na wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa wamefurika katika eneo la uwanja wa Ofisi ya CCM Mkoa huo wakifatilia kwa majini maelezo ya Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati alipokuwa akitoa shukrani kwa udhamini wa kishindo alioupata jana Juni 18, 2015.
Mh. Lowassa akisomewa Dua na Sheikh wa mji wa Moshi mara baada ya kupewa udhamini wa Kishindo katika Safari yake ya Matumaini.
Wadau wakipata taswira ya Mh. Lowassa wakati akiondoka kwenye Uwanja wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro.
Vijana wa CCM wa Mji wa Muheza wakiuongoza Msafara wa Mh. Lowassa kwenye eneo hilo la Muheza kwa lengo la kuzumza nao.
Vijana wa CCM Mji wa Muheza wakimshangilia Mh. Lowassa wakati walipomzimamisha ili aongee nao, alipokuwa safarini kuelekea Mkoani Kilimanjaro.
Ujumbe wa Vijana wa Muheza.
Ni furaha tupu.
Mh. Lowassa akiwasalimia wananchi wa Mji wa Muheza sambamba na kuwatakia Heri ya Mfungo Mtukufu wa Mwezi wa Ramadhani, wakati akiwa safarini kuelekea Mkoani Kilimanjaro kusaka wadhamini watakamuwezesha kupata ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni 18, 2015.
Baada ya kuwasalimia wanaCCM wa Mji wa Muheza, Mh. Lowassa alipata wasaa wa kwenda kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe, Mh. Adadi Rajab, Marehemu Mzee Rajab nyumbani kwao Muheza, Mkoani Tanga. anaezungumza na Mh. Lowassa ni Mama Mzazi wa Mh. Adadi Rajab, Bi. Fatuma Omar.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mh. Steven Ngonyani “Prof. Maji Marefu” (katikati) pamoja na wananchi wa Korogwe wakiwa wamefunga barabara kuuzuia msafara wa Mh. Lowassa ili aweze kuzungumza nao, huku wakimuuga mkono katika safari ya Matumaini.
Mh. Lowassa alishuka garini na kuungana na wananchi hao.
Mh. Lowassa akiwasalimia wananchi wa Mji wa Korogwe wakati akiwa safarini kuenekea Mkoani Kilimanjaro.
Shangwe tupu kwa wananchi wa Korogwe.
Kwaherini wana Korogwe.
Alipofika Mombo
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mh. Steven Ngonyani “Prof. Maji Marefu” akitoa neno.
Mh. Lowassa akitoa neno la shukrani kwa wakazi wa Mombo.
Mh. Lowassa akiwasalimia WanaCCM na Wananchi wa mji wa Hedaru.
Same.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mmoja wa Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonard Minja wakati alipofika kumpongeza kwa udhamini anaoendele kuupata.
No comments:
Post a Comment