Tuesday, June 16, 2015

MAPOKEZI YA MH. LOWASSA MJINI BUKOBA

 Sehemu ya Wakazi wa mji wa Bukoba Mkoani Kagera wakiwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Bukoba, wakimsubiri kumlaki Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa, tayari kwa kupokea fomu ya wanaCCM wa kumdhamini.
 Wadau wa CCM wakijadiliana jambo.
 Ndege iliyombeba Mh. Edward Lowassa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba, Mkoani Kagera.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Kagera, Mzee Pius Ngeze wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba, Mkoani Kagera jana Juni 15, 2015.
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Mh. Lowassa katika tabasamu.

  Umati wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera ukiwa umemzunguka Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa, wakati alipowasili kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Kagera, jana Juni 15, 2015.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Katibu wa UWT wilaya ya Bukoba Vijijini, Agness Bashemu alipokuwa akitoa taarifa fupi ya namna ya kumkabidhi fomu hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini, Yussuf Ngaiza.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete akiwasalimia wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera jana Juni 15, 2015.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoba, Dkt. Aman Kaborou akiwasalimia wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera jana Juni 15, 2015. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mngeja.
 Mjumbe wa Mkutano Mkuu (NEC) Bukoba, Nazir Karamagi akuzungumza machache mbele ya wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera jana Juni 15, 2015. 
 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Kagera, Mzee Pius Ngeze akizungumza mbele ya umati wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera jana Juni 15, 2015, na kutangaza kwamba yeye pia ni mmoja ya wana Safari ya Matumaini.
 Shangwe kila kona.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akipongezwa na Bibi huyu (ambaye jina lake halikuweza patikana kwa haraka) mara baada ya kupokea fomu za wanaCCM zaidi ya 6000 waliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.  
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Bukoba mjini, Acheni Mwinshehe, zenye majina ya wanaCCM wa Mkoa wa Kagera waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. 
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akizungumza na umati wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera jana Juni 15, 2015, Wakati akitoa shukrani zake kwa kumdhamini ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Zaidi ya wanaCCM 6000 wamdhamini mkoani Kagera.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akiwaaga wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera jana Juni 15, 2015, mara baada ya kupokea fomu za wanaCCM zaidi ya 6000 waliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. 

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...