Friday, February 06, 2015

JESHI LA POLISI NCHINI LASHIRIKI KUZINDUA MAGARI MAPYA YA KAMPUNI YA ULINZI YA SECURITY GROUP AFRIKA JIJINI DAR LEO

 Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la polisi
nchini Kamishina wa Polisi Mussa Ally Mussa akiwa na mkuu wa jeshi la polisi mstaafu
Philimon Mgaya akikata utepe wa kuashiria kuzindua magari mapya Zaidi ya
ishirini ya kampuni ya ulinzi ya Security Group Africa ambayo yataanza kutumika
katika kazi mbalimbali za kampuni hiyo hivi karibuni.Katikati yao ni mkurugenzi
mkuu wa kampuni hiyo Eric Sambu.
 Mwakilishi wa Mkuu wa jeshi la polisi
nchini 
Kamishina wa Polisi Mussa Ally Mussa  akipokea msaada wa pikipiki mbili aina ya
Boxer toka kwa mwenyekiti wa bodi wa kampuni ya Security Group Africa ambae pia
ni mkuu wa  jeshi la polisi mstaafu
Philimon Mgaya kwaajili ya kusaidia jeshi hilo katika oparasheni mbalimbali za
kupambana na uhalifu,Katikati yao ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SGA
nchini  Eric Sambu.
 Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SGA
nchini  Eric Sambu akizungumza kwenye
hafla ya kuzindua magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya
Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za kampuni
hiyo hivi karibuni.Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za kampuni hiyo Mbezi
Beach jijini Dar Es Salaam.
 Mwakilishi wa Mkuu wa jeshi la polisi
nchini 
Kamishina wa Polisi Mussa Ally Mussa  akikagua gwaride maalum la kuashiria
kuanza kwa shuguli ya kuzindua magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya
ulinzi ya Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali
za kampuni hiyo hivi karibuni.Kulia kwake ni mkuu wa kitengo cha mafunzo cha
SGA bwana Rogers Lumwaji.
 Mwakilishi wa Mkuu wa jeshi la polisi
nchini 
Kamishina wa Polisi Mussa Ally Mussa  akipeperusha bendera kuashiria kuanza
kutumika kwa magari magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya
Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za
kampuni hiyo hivi karibuni.Katikati yao ni mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Eric
Sambu.

No comments:

CCM ARUSHA WAUNGA MKONO AZIMIO, RAIS SAMIA NA RAIS MWINYI WAGOMBEA PEKEE 2025

  Na Vero Ignatus,Arusha MAELFU ya Wananchi wa Mkoa wa Arusha leo Jumamosi Februari 1, 2025 wamejitokeza kwa wingi kwenye tukio la kuung...