Kwaya Master Mwana FA akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo welcome pack jijini Mwanza jumamosi wiki hii.
Meneja Bidhaa wa Tigo Bw.Edwin Mgoa alisema kwamba kampeni hiyo ya Welcome Pack inayoendelea kwa muda wa mwezi mmoja na zaidi sasa imekwisha fanyika kwa mafanikio makubwa katika mikoa mingine ikiwemo Kagera, Kilimanjaro, Arusha, Iringa, Dodoma na Mbeya ambapo imewapa fursa maelefu ya wananchi kupata huduma za Tigo kwa karibu ikiwemo kifurushi cha Welcome Pack.
Kifurushi cha Welcome Pack, kwa mujibu wa Mgoa, kinampa mteja anaenunua laini mpya ya Tigo dakika 20 za muda wa maongezi, MB 175 za intanet, kutuma ujumbe mfupi wa SMS bila kikomo, na kiasi cha shilingi 500 kama salio la Tigo Pesa kwa kila mteja atakaye nunua laini ya Tigo kwa kiasi cha shilingi 1000 tu.
“Tumeandaa matamasha haya kwa ajili ya kusherehekea huduma hii mpya mahususi kwa wateja wetu. Na kwa safari hii, Tigo imeamua kwenda kutikisa jiji la Mwanza na kikundi cha The Orijino Komedi na wasanii wengine wa Bongo fleva. Kwa hiyo tunapenda kuwasihi wateja wetu wote wa kanda hiyo ya ziwa kuchukua fursa hii kuja kujaribu hii huduma yetu mpya pamoja na kupata burudani isiyo na kifani kutoka kwa wasanii bora kabisa kutoka nchini Tanzania,” alisema Mgoa.
Mmoja wa wanakikundi kutoka Orijino Komedi, Lucas Mhavile almaarufu kama Joti alisema kwamba yeye binafsi pamoja na kikundi chake kizima wanafuraha kubwa sana kushiriki katika msafara wa tamasha la Tigo Welcome Pack na wapo tayari kwenda Mwanza kuwapatia zaidi ya burudani mashabiki wao.
“Napenda kutoa rai kwa watu wote wa Mwanza kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa CCM Kiruma siku ya Jumamosi kuanzia saa 6 mchana. Tamasha la Tigo Welcome Pack si jambo la kukosa! Njoo upate burudani, ucheze na ufurahi. Lakini usisahau pia kujipatia kifurushi cha Welcome Pack kutoka Tigo na uanze kuwasiliana na marafiki na familia yako kupitia ofa kabambe kabisa kutoka Tigo,” alisema Joti.
Akifafanua kuhusu kifurushi cha Welcome Pack, Mgoa alisema kwamba kifurushi hicho kinakuja na dakika 20 za muda wa maongezi, MB 175 za intanet, kutuma ujumbe mfupi wa SMS bila kikomo, na kiasi cha shilingi 500 kama salio la Tigo Pesa kwa kila mteja atakaye nunua laini ya Tigo kwa kiasi cha shilingi 1000 tu.
“Hii itawawezesha wateja wetu kuwasiliana zaidi na kwa gharama nafuu ambayo haijawahi kutokea,” alisema Mgoa.
Kampeni ya Welcome Pack itakuwepo kwa muda wa miezi mitatu, ambapo misafara zaidi ya 70 ikiwemo basi la Tigo la Kidijitali lenye malengo la kuwaelimisha wateja kuhusu huduma za Tigo za kidijitali litatembelea miji 70 na vijiji zaidi ya 100 ndani ya mikoa 10 tofauti ikiwemo Mbeya, Iringa, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Kigoma na Mtwara.
Wasanii maarufu wa Bongo fleva watakaotoa burudani ni pamoja na Profesa J, Joh Makini, Shah, Mheshimiwa Temba na Chege, Madee na Izzo Business. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwakaribisheni nyote,” alimalizia kwa kusema Mgoa.
No comments:
Post a Comment