Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana akinyanyua mikono juu kuashiria mshikamano na baadhi ya viongozi wa makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan Kusini ambao wako kwenye mgogoro wa kugombea madaraka kwa takribani mwaka sasa. Kinana amekutana na viongozi hao wakati wa mkutano wa hadhara mjini Masasi, Mtwara baada ya kumfuata na kutaka ushauri wa upatanishi nchini kwao Sudani Kusini. Baada ya viongozi hao kupata wasaa wa kusalimiana na wananchi katika mkutano huo uliofanyika mjini Masasi Baadae Kinana alifanya nao mazungumzo Ikulu Ndogo ya Masasi. Viongozi hao wamemfuata Kinana mjini Masasi kutokana na kwamba yuko katika ziara ya kikazi ya mikoa ya Lindi na Mtwara akiendelea na shughuli za kuimarisha Chama hicho na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE- MASASI)
Viongozi wa vikundi hivyo wakiwa mjini katika mkutano wa CCM mjini Masasi
Kinana akizungumza na viongozi hao ikulu ndogo mjini Masasi
Katika ziara yake inayoendelea mkoani Mtwara Kinana alitembelea kiwanda cha kubangua korosho na kujieonea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo hapa akionyesha wa mashine ya kufunga korosho.
Baadhi ya akina mama wafanya kazi wa kiwanda hicho wakichambua korosho na kuzitenga katika madaraja
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mashine za kisasa za kubangua korosho
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza baada ya kukagua kiwanda hicho kinachomilikiwa na mama Kate Kamba. kulia
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Afisa Ushirika wa Mkoa wa Mtwara Bw. John Henjewele kuhusu matatizo ya korosho kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Makaravati katika barabara ya Migongo mjini Masasi
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kufyatua matofali katika eneo la litakalojengwa ofisi mpya ya CCM baada ya ile ya zamani kuchomwa katika vurugu zilizotokea mwaka jana mjini Masasi
Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Bw. Shaibu Akwilombe akizungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika uwanja wa Fisi.
Nape Nnauye akizungumza na wananchi katika uwanja wa Fisi mjiji Masasi
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa mavazi ya kimila na wazee wa kabila la wamakonde kama ishara ya kumpa heshima ya kabila hilo.
Wananchi wakifurahia jambo katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Mbunge wa jimbo la Masasi Mariam Kasembe akizungumza na wapiga kura wake.
No comments:
Post a Comment