Wednesday, November 26, 2014

AIRTEL YAJA NA UNI255 KUTOA FURSA KWA WANAFUNZI VYUO VIKUU KUFAIDI INTANET KWA GHARAMA NAFUU KULIKO ZOTE

 Mkurugenzi wa Airtel Huduma kwa Wateja,Bi.Adriana Lyamba akimkabidhi kombe Nahodha wa timu ya Simba ya UDOM kwa kuibuka washindi wa mashindano ya Airtel Uni 255,yaliyofanyika katika viwanja vya michezo ndani ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),Mashindano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
 Timu ya Simba ikishangilia mara baada ya kukabidhiwa kombe lao mara baada ya kuibuka kinara katika mashindano ya Soka ya Airtel 255.
 Aidha Aneth Mugha ambaye ni Meneja Masoko wa Airtel alikifafanua mbele ya Wanafunzi wa UDOM (hawapo pichani),namna vocha mpya
ya Airtel Uni 255 inavyoweza kuwanufaisha katika suala zima la kuperuzi kwa gharama nafuu kuliko
zote wakiwa chuoni hapo.Bi, Aneth alisema kuwa Airtel Uni 255 ni huduma
maalum kwa vyuo vikuu inayomuwezesha mwanafunzi kupata huduma nafuu ya
mawasiliano ikiwemo kupiga simu, sms, na intanet ili kwasaidia wanafunzi
kutumia huduma hiyo kujiendeleza kimasomo.
 Baadhi ya Wanafunzi wakishuhudia burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye jukwaa la Airtel Uni 255,baada ya mashindano ya Soka kumalizika na kumpata mshindi,Wasanii waliotoa burudani kwenye jukwaa hilo ni Roma,Ney wa Mitego pamoja na Vanessa Mdee a.k.a V-Money na burudani nyingine,ambapo wasanii chipukizi walishindana kughani na kuibuka na zawadi mbalimbali zikiwemo simu za mikononi,fulana na nyinginezo.
 Baadhi ya Wanafunzi wa chuo cha Dodoma (UDOM) wakiwa jukwaa wakijiunga na huduma maalum ya UN 255,ambayo imetolewa kwa ajili yao.Airtel Uni 255 ni huduma
maalum kwa vyuo vikuu inayomuwezesha mwanafunzi kupata huduma nafuu ya
mawasiliano ikiwemo kupiga simu, sms, na intanet ili kwasaidia wanafunzi
kutumia huduma hiyo kujiendeleza kimasomo.
Aidha Aneth Mugha ambaye ni Meneja Masoko aliwatangazia Wanafunzi wa UDOM,namna vocha mpya
ya Airtel Uni 255 inavyoweza kuwafaidisha kuperuzi kwa gharama nafuu kuliko
zote wakiwa chuoni hapo.
 Baadhi ya Wanafunzi wa UDOM wakishangilia burudani iliyokuwa ikitolewa kweye jukwaa la burudani la Airtel Uni 255,ambapo wasanii mbalimbali walitumbuiza akiwemo Ney wa Mitego,Roma Mkatoliki pamoja na Vanessa Mdee a.k.a V-Money.
Sehemu ya umati wa wanafunzi wa UDOM wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri jukwaani kwa usiku huo wa tamasha la Airtel Uni255
Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la
kisanii Ney wa Mitego akitumbuiza kwenye tamasha la Airtel Uni 255, lililofanyika
katika viwanja vya michezo ndani ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),Mashindano
hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la
kisanii Roma Mkatoliki  akitumbuiza
kwenye tamasha la Airtel Uni 255, lililofanyika katika viwanja vya michezo
ndani ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),Mashindano hayo yalifanyika mwishoni mwa
wiki mkoani Dodoma.
Meneja Mahusiano waAirtel Tanzania,Jakson Mmbando akitoa maelekezo mafupi mbele ya Wanachuo (hawapo pichani) kuhusiana na shughuli nzima ya tamasha laAirtel Uni 255, lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya michezo
ndani ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),mkoani Dodoma.
Kikosi cha timu Yanga  ya UDOM wakiwa katika picha ya pamoja,ambao waliibuka washindi wa pili wa mashindano ya Airtel Uni
255,yaliyofanyika katika viwanja vya michezo ndani ya Chuo kikuu cha
Dodoma (UDOM),Mashindano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani
Dodoma.
 Mmoja wa Wanafunzi mzuka ukiwa umempanda vyama kabisa wakati msanii wa muziki wa kizazi kipya Ney wa Mitego alipokuwa akitumbuiza kwenye tamasha la Airtel Uni
255.
Mmoja wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Vanessa Mdee a.k.a V-Money akiwaimbisha wanafunzi wa chuo cha UDOM,kwenye tamasha la  Airtel Uni
255 lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
 Sehemu ya umati wa wanafunzi wa UDOM wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri jukwaani kwa usiku huo wa tamasha la Airtel Uni255

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...