Tuesday, November 18, 2014

ABDULRAHMAN KINANA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI NCHINGA, SAID MTANDA MAMBO YAKE SAFI

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Nchinga mkoani Lindi Mh. Said Mtanda wakati alipowasili katika Kitomanga kata ya Mkwajuni ambapo pia alishiriki katika shughuli za ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao linalojengwa katika kijiji hicho, Katibu Mkuu wa CCM yuko katika ziara ya siku 16 katika mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali kwa pamoja na wananchi huku akihimiza uhai wa chama, Katika ziara hiyo Kinana ameongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NCHINGA -LINDI)2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumpokea katika kata ya Mkwajuni jimbo la Nchinga jana.3Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Lindi Dkt, Nassoro Ally Hamidi wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili katika jimbo la Nchinga.4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akimsikiliza Mbunge wa jimbo la Nchinga Mh. Said Mtanda wakati akizungumza na wananchi wa jimbo lake.5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akizungumza mara baada ya mapokezi hayo huku mbunge wa jimbo hilo Mh. Said Mtanda na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakifurahia jambo.6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akishiriki ujenzi wa ghala katika kata ya Mkwajuni huku mbunge wa jimbo hilo Mh Said Mtanda akishuhudia.7Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi hayo.8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa kwa matawi ya miti na wananchi wa Mipingo Namkongo katika jimbo la Nchinga.9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiagalia mashimo ambayo akina mama waliokuwa wakichimba ili kupata maji ya kutumia katika kijiji chao lakini kwa sasa tatizo hilo limeshakwisha baada ya mradi wa maji kukamilika katika kijiji hicho.10Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi mifuko ya saruji Muhaji Mtondo Afisa Mtendaji wa kijiji cha Namkongo kwa ajili ya kusakafia soko katika kijiji hicho, katikati ni Mbunge wa jimbo la Nchinga Mh. Said Mtanda aliyetoa saruji hiyo.11Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji pamoja na Mbunge wa jimbo Nchinga Mh. Said Mtanda wakifugua maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji uliogharimu shilingi milioni 166 mpaka kukamilika katikati ni  Mkuu wa mkoa wa Lindi Ndugu Magalula Said Magalula.13Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza wakati Katibu Mkuu wa CCM alipowasili katika kata ya Kilangala jimbo la Nchinga.15Mbunge wa jimbo Nchinga Mh. Said Mtanda  katikati Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika kata ya Kilangala.16Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi baiskeli zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Nchinga kwa viongozi wa CCM wa kata kwa moja wa viongozi hao Bw.Samwel Kibena kutoka kata ya Kilangala.19Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na watendaji wa halmashauri ya mkoa wa Lindi wakati alipotembelea ujenzi wa zahanati ya Nchinga II.20Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka mara baada ya kukagua ujenzi wa zahanati ya Nchinga II mkoani Lindi.21Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi wa kata ya Milola jimbo la Nchinga.22Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Milola.23Mbunge wa jimbo Nchinga Mh. Said Mtanda  akifafanua jambo kuhusu hatua zilizopigwa kwa maendeleo ya jimbo la Nchinga wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Milola.24Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano huo.25Mbunge wa jimbo la Mtama na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mkoa wa Lindi Mh. Bernard Membe akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Milola jimbo la Nchinga mkoani Lindi jana.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...