Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiponda mawe wakati aliposhiriki katika ujenzi wa Bwawa la maji linalojengwa katika kijiji cha Sengenya Mangaka wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara akiwa katika ziara yake ya kikazi akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali pamoja na wananchi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuhimiza uhai wa chama cha Mapinduzi CCM, Katika ziara hiyo leo Kinana amefanya kazi mbalimbali pamoja na kufanya mikutano kadhaa akiwa ameongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NANYUMBU-MTWARA)Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na mafundi kupanga mawe katika ukingo wa bwawa hilo linalojengwa katika kijiji cha Sengenya Mangaka wilayani Nanyumbu.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo wakati alipokuwa akikagua kituo cha afya cha Mangaka wilayani Nanyumbu ambapo ameelezwa kwamba kituo hicho kimeomba kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ya wilaya ambapo kimekidhi vigezo vyote lakini wamesubiri kwa miaka mitatu bila mafanikio.Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo akizungumza na waandishi wa habari adha wanayoipata wagonjwa kutokana na kutopandishwa hadhi na kuwa hospitali ya wilaya pamoja na kukidhi vigezo vyote vya kuwa hospitali ya wilaya.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo katika chumba cha upasuaji kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo mara baada ya kutembelea kituo hicho katikati ni Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo S. Kiswaga.Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi, Mh. Festus Kiswaga Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu na Halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Mtwara wakipita kwenye daraja la UmojaNi Daraja lenye urefu wa zaidi ya mita 700.Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani, Mh. Festus Kiswaga Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu na Halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Mtwara wakipita kwenye daraja la UmojaMkurugenzi wa mtandao huu wa Fullshangwe akivinjari katika daraja hilo.Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata picha ya kumbukumbu na wanahabari walioko katika msafara wake.Shehena ya mbao ziliokamatwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita zikiwa zimehifadhiwa katika ofisi za Mamlaka ya mapato TRA Mtambaswala katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji.Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari kuelezea uzembe na ukiritimba wa baadhi ya watumishi wa serikali kutokana na suala hilo kuchukua muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi.Halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Mtwara akizungumza na wananchi katika kijiji cha Nanyumbu Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akizungumza na wananchi katika kijiji cha Nanyumbu
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi , Mh. Festus Kiswaga Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu na Halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Mtwara wakipita kwenye daraja la Umoja.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Nanyumbu.
No comments:
Post a Comment