Sunday, November 02, 2014

DK. KIGWANGALA AHIMIZA AMANI NCHINI

1Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akizungumza na vikundi mbalimbali mbalimbali vya Joging vilivyoshiriki katika tamasha la Mbio za Amani lililoshirikisha wawakilishi kutoka pande mbalimbali za nchi na kupokelewa na mbunge huyo ambye alikuwa mgeni rasmi, Dr. Khamis Kigwangala amewaasa wanasiasa kutoleta siasa za uchochezi hasa katika mchakato mzima wa Katiba mpya ambapo amesema waachwe wananchi wenyewe waisome waielewe na wao wataamua kama wataipigia kura ya Ndiyo au Hapana, mapokezi hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)2Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akijitolea damu kwa kitengo cha Damu salama ambacho kikilishiriki sambamba na tamasha hilo kuhamasisha wanamichezo hao ili wajitolee damu katika kuokoa maisha ya wahitaji wa damu.3Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akishiriki katika zoezi la viungo mara baada ya kupokea vikundi hivyo vya Jogging kutoka maeneo mbalimbali nchini.4Kutoka kushoto ni Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo BMT Bw. Dioniz Malinzi na Bw. Jimmy mmoja wa viongozi wa shirikisho la vyama vya Jogging wakishiriki kuimba wimbo wa taifa katika tamasha hilo.5Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akishiriki katika mazoezi6Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akipokea vikundi vya Jogging katika viwanja vya Mnazi Mmoja mara baada ya kumaliza mbio za Amani.7Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akipokea vikundi vya Jogging katika viwanja vya Mnazi Mmoja mara baada ya kumaliza mbio za Amani.8Bw.Abdulla Mohamed Mwenyekiti wa Mipango ya Maandalizi ya tamasha hilo akimkabidhi jenzi Mwenyekiti wa Barza la Michezo BMT Bwa Dioniz Malinzi.9Mdau wa michezo na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Kanali Mstaafu Iddi Kipingu akizungumza na vikundi hivyo.1011Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akishiriki kuchezo kigoma cha Amani mara baada ya kupokea vikundi vya Jogging katika viwanja vya Mnazi Mmoja.12Bw. Dioniz Malinzi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo BMT akizungumza jambo na vikundi hivyo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Tamasha la Mbio za Amani.13Vikundi hivyo vikifanya mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja.14Vikundi hivyo vikiimba wimbo wa Taifa.
……………………………………………………………..
Wanasiasa wameaswa kudumisha amani, upendo na mshikamano wa Tanzania, ili kuepuka vurugu zinazoweza kujitokeza ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikisababishwa na makundi ya wanasiasa, kwa kutoa ujumbe kwa wananchi unao chochea kuvurugukika kwa amani ya Tanzania.
Akizungumza na wanamichezo wa vilabu mbalimbali vya kukimbia (Jogging) kutoka Tanzania bara na Zanzibar, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,  mbunge wa jimbo la Nzega, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Tawala za mikoa na seikali za mitaa, Dk. Hamis Kigwangala, amesema wakati bunge maalum la Katiba lilipokuwa likitunga katiba inayopendekezwa, kuliibuka baadhi ya wanasiasa, waliokana kushiriki katika bunge hilo na kutofautiana  katika baadhi ya mambo kuingizwa katika katiba hiyo, huku wale waliobaki ndani ya bunge maalumu la katiba  kwa asilimia takriban 85 wakiheshimu maamuzi ya watanzania na kuhakikisha katiba mpya inapatikana.
Hivyo amewataka wanasiasa pamoja na kuwa mapendekezo yao hayakuingia ndani ya katiba wasiwe chanzo cha kutokuridhika kwao kulazimisha na watanzania wengine wasiridhike na kwamba watanzania waachwe siku ya kuipigia kura katiba inayopendezwa itakapo tangazwa, watanzania waipigie kura ya ndio au hapana na kwamba waamue kwa utashi wao bila uchochezi wa wanasiasa.
Katika Tamasha hilo lililopewa jina la Mbio za amani 2014, Dk, Kigwangala pia amehimiza umuhimu wa kufanya michezo kila wakati, kwani michezo ni Afya, Furaha, Amani, Upendo na Ajira, huku akivitunuku vyeti baadhi ya vilabu vya Jogging kwa kushiriki katika tamasha hilo.
Tamasha hilo limeshirikisha wanamichezo wa vilabu vya Jogging kutoka Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam, ambapo limeandaliwa na Faita Jogging & Sports Club ya jijini Dar es Salaam, huu ukiwa ni mwaka wa tatu kuandaliwa.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...