Kwa mwananchi yoyote ambaye hajafungwa kimawazo na kifikra, angalia vizuri hii video kwenye dakika ya 1:18 ili yale uliyoambiwa uchanganye naya kwako kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kwa Paulo Makonda!.

Mtoa mada katika mdahalo wa kujadili Katiba Inayopendekezwa, Jaji Joseph Warioba akitoa mada kabla ya mkutano huo kuvunjika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Saam.
Jaji Joseph Warioba akitoa mada katika kongamano kabla ya vurugu kutokea.

Baadhi ya vijana walioingia na mabango ndani ya ukumbi wa mkutano wakionyesha mabango yao.

Jaji Joseph Warioba akiangalia usalama wake kabla ya kuondolewa na mlinzi wake katika ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo mdahalo wa kuijadili Katiba Inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika kabla ya kuvunjika.


Mlinzi wa Jaji Joseph Warioba (kushoto) akimkinga kwa mikono ili asipate madhara baada ya kuanza vurugu katika mdahalo wa kujadili Katiba Inayopendekezwa. 



Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole akiongea na mmoja wa vijana aliyekuwa na jazba mara baada ya kutokea kwa vurugu katika mdahalo wa kujadili Katiba Inayopendekeza.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku (katikati) akisindikizwa kuingia katika chumba cha VIP mara baada ya kuvunjika kwa mdahalo wa kujadili Katiba Inayopendekezwa.





Baadhi ya vijana wakionyesha mabango yenye ujumbe mbali mbali

Paulo Makonda akimsaidia mlemavu wa macho, Amon Mpanju baada ya vurugu kuanza kutokea ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza.



Baadhi ya viti vilivyotumika kama silaha na kinga kwenye vulugu


Jaji Warioba akitoka katika ukumbi huku akisindikizwa na askari kanzu.

Jaji Warioba akisindikizwa na makachero wa Polisi baada ya kuvunjika kwa mdahalo wa Katiba Inayopendekezwa