Tuesday, November 04, 2014

MCHAKATO WA TUZO ZA WANAWAKE WENYE MAFANIKIO TANZANIA WAZINDULIWA RASMI LEO JIJINI DAR

Rais wa Taasisi ya kijamii ya Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (Tanzania Women of Achievement ),Bi. Irene Kiwia (kulia) akisisitiza jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani) juu ya utoaji wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania ambazo zitafanyika Machi 7,2015 kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake, ikiwa na lengo la kuwatambua na kuwapongeza wanawake ambao wamechangia maendeleo ya nchi katika nyanja tofauti.…
Rais wa Taasisi ya kijamii ya Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (Tanzania Women of Achievement ),Bi. Irene Kiwia (kulia) akisisitiza jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani) juu ya utoaji wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania ambazo zitafanyika Machi 7,2015 kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake, ikiwa na lengo la kuwatambua na kuwapongeza wanawake ambao wamechangia maendeleo ya nchi katika nyanja tofauti.
Mwenyekiti wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA), Mama Sadaka Gandhi (katikati) akitoa ufafanuzi juu ya namna Tuzo hizo zitakavyokuwa zikitolewa na wanaohusika kupewa tuzo hizo,wakati wa mkutano na wanahabari (hawapo pichani) uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena,Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Taasisi ya kijamii ya Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (Tanzania Women of Achievement ),Bi. Irene Kiwia na kushoto ni Katibu Mkuu wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA),Bi. Hellen Kiwia.
Katibu Mkuu wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA),Bi. Hellen Kiwia akielezea namna ya wanawake watakavyoshiriki ili kuweza kupata Tuzo hizo.
Sehemu ya Waandishi wa habari waliohudhulia Mkutano huo.
Timu nzima ya Taasisi ya kijamii ya TWA (Tanzania Women of Achievement ) inayoratibu utoaji wa tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...