Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitembelea maghala ya kuhifadhia korosho wilayani Tandahimba, Mtwara wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi na kupkea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kinana akisaidia kumtwisha gunia la korosho mmoja wa wapagazi wa maghala ya kuhifadhia korosho, wilayani Tandahimba.
Kinana akikagua mradi wa maji wa Mkupete katika Kata ya Mahuta.
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Mdimba, wilayani Tandahimba
WANANCHI wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika Kata ya Mahuta, wilayani Tandahimba
Kinana akitembelea baadhi ya nyumba 100 zilizoezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa katika Kijiji cha Nanyanda, wilayani Tandahimba
Kinana akiwafariji baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Nanyanda ambao wameathirika baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo wa mvua
Kinana akiendelea kukagua nyumba hizo zilizoezuliwa
Kinana akipandisha bendera katika Shina la CCM la wakereketwa mjini Tandahimba
Kwaya ikitumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara Mjini Tandahimba
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF wa Kata ya Kitama akipongezwa na Kinana baada ya kuhamia CCM katika mkutano huo wa hadhara. Hivi sasa ni Mkobo ni Green Guard wa CCM Wilaya ya Tandahimba
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Tandahimba ambapo alimtaka Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad aache kuwahadaa wananchi kwamba wasiipigie kura Katiba inayopendekezwa akidai ni ya CCM na kwamba akitaka kuwa mkweli aachie ngazi nafasi ya Umakamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya CCM inayoongozwa na CCM
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, akielezea utekelezji wa miradi mbalimbali jimboni humo wakati wa mkutano huo wa hadhara.
No comments:
Post a Comment