Majembe ya Skylight Band yakitoa burudani ya kukata na shoka kwa mashabiki wao Ijumaa iliyopita ndani ya ukumbi wa Thai Village Masaki jijini Dar..Kutoka kushoto ni Aneth Kushaba AK47, Mkongwe wa muziki wa dansi Joniko Flower, Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa bongo, Digna Mbepera na Sam Mapenzi.
Sehemu ya umati wa mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na sebene la Nasaka Dough ndani ya kiota cha Thai Village Masaki Ijumaa iliyopita.
Kikosi kazi cha Skylight Band kikiongozwa na rapa Joniko Flower kutoa burudani kwa mashabiki wake (hawapo pichani) Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha maraha cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Kutoka kushoto ni Aneth Kushaba AK47, Sony Masamba, Bela Kombo, Sam Mapenzi na Digna Mbepera wakijibu mapigo ya mashabiki wa Skylight Band kwa staili ya aina yake.
Mashabiki wa Skylight Band wakijibu mapigo kwa staili ya “Yachuma chuma”…Muguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma, Yachuma chuma nataka mukanda Yachuma chuma….raha iliyoje unakosaje sasa, fanya uje tukutane pale kati.
Divas wa Skylight Band wakiongozwa na Meneja wa bendi Aneth Kushaba AK47 kutoa burudani kwa mashabiki wao. Kulia ni Bela Kombo na kushoto ni Digna Mbepera kwenye show iliyowabamba wakazi wa jiji la Dar Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village Masaki jijini Dar.
No comments:
Post a Comment