Saturday, January 23, 2010

Wawakilishi Zanzibar


Spika wa baraza la wawakilishi, Pandu Ameir Kificho akisalimiana na mwakilishi wa viti maalum wanawake CUF, Zakia Omar. kulia ni mwakilishi wa Bububu, Khatibu Suleiman bakari nje ya ukumbi wa baraza la wawakilishi.

Kumekuwa na udhaifu katika kutunza mazingira yanayobeba vivutio vya utalii katika mji mkongwe wa Zanzibar kama picha inavyoonyesha kaburi la mfanyabiashara maarufu wa enzi hizo, Tiptip lilivyoachanizwa na sehemu hiyo baadhi ya watu wamefanya dampo la takataka ambapo watalii wengi baada ya kutembelea nyumba yake Shangani pia huzuru kwenye kaburi hilo.

Waziri wa katiba na utawala bora, Ramadhan Abdalla Shaaban (kushoto) akibadilishana mawazo na mwakilishi wa Ole, Hamad Omar Masoud (kati) na Assaa Othman Hamad wa Wete nje ya ukumbi wa baraza la wawakilishi jana. picha zote na Martin Kabemba.

Wajumbe wa baraza la wawakilishi wakifurahia jambo baada ya kuahirishwa kwa kikao cha asubuhi. kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi na wawakilishi wa CUF, Juma Haji Duni na Nassor Ahmed Mazrui jana.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...