Sunday, January 03, 2010

Maisha Plus 2010




Msimu wa pili wa maisha ya kijiji cha plus umeanza rasmi usiku wa mkesha wa mwaka mpya kwa fainali na washiriki 18 wameingia kijijini kuianza safari ya siku zisizopungua 56.


Msimu huu ulioanza kwa usaili katika maeneo 13 ya Tanzania bara na visiwani,ulianza mwezi wa nane kwa kuchagua washiriki kumi bora ya kila mkoa kutoka katika maelfu ya washiriki waliojitokeza.


Baada ya washiriki kumi kuchaguliwa na waandaaji, majina hayo kumi yalipelekwa kwa watazamaji ambao walipiga kura kuchagua 3 bora ya kila mkoa. Jumla ya washiriki walioingia tatu bora za maeneo yote ni 42 ambapo tanga ilitoa
washiriki wawili badala ya watatu kutokana na matatizo binafsi ya mshiriki mmoja. Zanzibar imetoa washiriki wanne badala ya watatu kutokana na kupewa heshima ya kutoa mshindi wa msimu wa kwanza.

Dar es salaam nayo imetoa washiriki 6 kutokana na kuunganishwa na mkoa wa Pwani. Marafiki wema waliosaidia msimu wa pili wa maisha plus ni city style hotel iliyoko sinza, infinity communications na aurora.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...