Monday, January 11, 2010
Kipawa wazuia skuli kubomolewa
WAKATI muda uliowekwa na serikali kwa watu wa Kipawa, jijini Dar es Salaam, kuyahama makazi yao ukamalizika leo, wananchi hao wamezuia mpango wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, kutaka kubomoa majengo ya Shule ya Msingi ya Kipawa.
Kwa sasa, majengo hayo ya shule yamekuwa yakitumika kama makadhi ya muda kwa baadhi ya wananchi hao ambao nyumba zao zilianguka baada ya serikali kulitwaa eneo hilo kwa ajili ya upanuzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa wa Julius Nyerere.
Hatua ya wananchi hao kuzuia kuvunjwa kwa majengo ya shule hiyo iliyoko karibu na uwanja wa ndege, ilifanywa jana kwa madai kuwa waliotumwa kwenda kufanyakazi hiyo, hawakujitambulisha na kwamba inawezekana kuwa ni genge la wezi.
Mmoja wa wananchi hao, Elias Justine, alisema kitendo cha watu wasiojulikana kwenda katika eneo hilo kwa lengo la kutaka kubomoa majengo bila ya barua kutoka serikarini ni cha hatari kwa sababu kuna uwezekano kuwa watu hao ni wezi.
.
“Sisi hatuwatambui watu hawa kama tutawaacha wafanye kazi hii, wanaweza kutuingiza majaribuni na kuonekana kuwa watu wa Kipawa ni wezi, tumeiba mabati ya majengo ya shule,nawaomba muachane na kazi hii,”alisema Justine.
Alisema eno hilo bado linakaliwa na watu ambao kimsigi, wanasubiri kupata haki zao kupitia mahakama na kwa hiyo, si busara majengo hayo kubomolewa.
Akisimulia tukio hilo,Halima Mohamed, alisema aliona kundi la watu wakiwa kwenye magari na baadaye, waliteremka na kujitambulishwa kuwa ni walimu.
Mkurugenzi wa Manispa ya Ilala Gabriel Fuime alilimbia Mwananchi kuwa kulingana na notisi ya serikali, muda wa kubomoa majengo katika eneo hilo umewadiwa.
“Mimi nilishalipwa fidia na (Taa) na nilishapewa notsi ya kutakiwa kubomoa jengo langu, muda wa notisi hizo umeisha na siwezi kukubali Taa waje wabomoe kwa sababu wataharibu mali zangu," alisema.
Fuime alisema lengo la kubomoa majengo hayo ni kutaka kuchukua mali na samani zilizopo ili zikasaidie kukarabati na vyoo na majengo ya shule jirani. Imeandikwa na Geofrey Nyang’oro wa Mwananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
TUME YA MADINI YAAINISHA MIPANGO YA KUWAWEZESHA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI
Uanzishwaji wa masoko ya madini wapunguza utoroshwaji wa madini Elimu yatolewa kwa wachimbaji wadogo wa madini CHUNYA Ikiwa ni mkakati wa k...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment