Sunday, January 10, 2010

Togo yajiondoa kwenye michuano ya CAF


Mchezaji wa Togo Emmanuel Adebayor

Timu ya taifa ya Togo imejitoa kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika huko Angola baada ya tukio la kushambuliwa kwa risasi na kusababisha vifo.
Dereva wa basi, kocha msaidizi na afisa habari waliuawa. Wachezaji wawili waliuawa katika shambulio hilo lililotokea siku ya Ijumaa katika mkoa wa Cabinda.
Waandaaji wanasisitiza kuwa michuano itaendelea na kwamba wataimarisha usalama.
Lakini mchezaji wa Togo, Alaixys Romao, ameliambia gazeti moja la lugha ya kifaransa L'Equipe: "Tunazungumza na timu nyingine katika kundi letu kuzishawishi zisusie."
Katika mechi yao ya kwanza siku ya Jumatatu, Togo ilipangiwa kucheza na Ghana huko Cabinda na wachezaji wa timu hiyo inayojulikana kama Black Stars wamesema kuwa wako tayari kuendelea kucheza.
Ivory Coast na Burkina Faso ni timu nyingine zilizopangwa katika kundi B.
www.bbcswahili.com

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...