Michuano ya CAN 2010 inaanza leo Angola



Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, CAN 2010 inaanza leo Jumapili nchini Angola kwa mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji dhidi ya Mali itakayochezwa mji mkuu Luanda.

Ulinzi umeimarisha na waandaaji wamesema mashindano yatasonga mbele licha ya shambulio la bunduki dhidi ya timu ya taifa ya Togo lililotokea katika ardhi ya Angola.

Ratiba na matokeo Dereva wa basi, kocha msaidizi na afisa habari waliuawa. Wachezaji wawili waliuawa katika shambulio hilo lililotokea siku ya Ijumaa katika mkoa wa Cabinda.

"Kipaumbele kwetu ni usalama wa wachezaji, lakini mashindano yatasonga mbele," alieleza msemaji wa shirikisho la soka barani Afrika, CAF.

Mechi zitakuwa zikifanyika mji mkuu Luanda, Cabinda, Benguela na Lubango.

Katika mechi yao ya kwanza siku ya Jumatatu Togo ilipangiwa kucheza na Ghana huko Cabinda na wachezaji wa timu hiyo inayojulikana kama Black Stars wamesema kuwa wako tayari kuendelea kucheza.

Comments