Thursday, January 14, 2010
Maalim Seif ataka uchaguzi usogezwe mbele
KATIBU mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amependekeza uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka huu usogezwe mbele au Rais Amani Abeid Karume aongezewe muda ili kuweka misingi imara ya kuondoa siasa za chuki visiwani humu.
Hamad alitoa pendekezo hilo jana alipokuwa akiwasilisha mada kwenye kongamano la siku moja la kujadili maridhiano na mustakabali wa Zanzibar lililofanyika kwenye Hoteli ya Bwawani mjini Unguja.
Pendekezo hilo limekuja siku mbili baada ya Rais Amani Abeid Karume kueleza kwenye sherehe za Mapinduzi kuwa hakuna muhula wa tatu kwa urais wa Zanzibar katika hotuba iliyoonekana kama ya kuaga Wazanzibari.
Wakati Karume akionekana kukataa pendekezo hilo ambalo utekelezaji wake unahitaji mabadiliko ya kikatiba, Maalim Seif aliibuka na wazo tofauti katika kongamano hilo lililoandaliwa na chama chake na kushirikisha viongozi mbalimbali wa kisiasa, dini, wasomi na wataalamu wa ndani na nje ya nchi.
”Binafsi nimekuwa nikitafakari sana changamoto hizi na naamini tunapaswa kuzitafakari na kuzijadili kwa lengo la kuona tunazikabili vipi," alisema Seif ambaye aliwahi kuwa waziri kiongozi. Habari hii imeandikwa na Salma Said, Zanzibar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment