Wednesday, January 13, 2010

Wapiga debe nomaaaa





LICHA ya juhudi ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam ya kuwakamata wapiga debe na wanaokatisha tiketi nje ya kituo ya kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo kama inavyoonekana hapo juu katika picha, hali ya usalama katika kituo hicho bado ni tete.
Mwananchi ilishuhudia wapiga debe na wakatisha tiketi wakiendelea kufanya shughuli hizo bila ya woga wowote huku wakiwasumbua abiria waliokuwa walifika kituoni hapo huku wimbi la matukio ya utapeli likiongezeka.
WAkizungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini baadhi ya watu wanaofanya shughuli zao katika kituo hicho wamesema operesheni ya kuwaondoa wapiga debe na wakatisha tiketi inakuwa ngumu kutokana na baadhi ya wamiliki wa mabasi yaliyopo kituoni hapo kuwalinda wapiga debe hao.
“Hapa wapiga debe na wakatisha tiketi hawawezi kuondoka kwa sababu hawa wamiliki wa mabasi wamekuwa wakiwalinda kwani wakikamatwa uenda kuwatoa sasa hii hali unafikiri itaisha kweli”,alisema mfanyabiasha wa vocha za simu kituoni hapo.
Walisema kuwa kituo hicho kimekuwa ni sehemu ya matapeli na vibaka kufanyia uhalifu wao kwani kila mara abiria wamekuwa wakiibiwa ama kutapeliwa kituoni hapo.
Mmoja wa wapiga debe wa kituo hicho alisema kuwa wao shughuli hiyo ndiyo inayowaingizia kipato hivyo wataendelea kufanya kazi hiyo licha ya kukamatwa na polisi. Imeandikwa na Masoud Masasi.

No comments:

TUME YA MADINI YAAINISHA MIPANGO YA KUWAWEZESHA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

Uanzishwaji wa masoko ya madini wapunguza utoroshwaji wa madini Elimu yatolewa kwa wachimbaji wadogo wa madini CHUNYA Ikiwa ni mkakati wa  k...