Friday, January 29, 2010

LEO NI LEO JIJINI KAMPALA:R.KELLY IS IN TOWN


Mashabiki wa muziki,hususani wa R&B waliopo katika ukanda wa Afrika Mashariki na hususani jijini Kampala nchini Uganda,huenda leo wakashuhudia onyesho ambalo hawajashuhudia ndani ya miaka kadhaa na huenda wasishuhudie katika miaka kadhaa ijayo.Hiyo ni ahadi,sio kutoka kwa bongocelebrity bali kutoka kwa mwanamuziki Robert Sylvester Kelly maarufu kama R.Kelly(pichani) kutoka nchini Marekani anayetarajiwa kufanya onyesho la aina yake hapo leo jijini Kampala katika ukumbi wa Lugogo Cricket Oval.


Onyesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya simu ya Zain,limepewa jina la “I Believe”.Hivi karibuni iliarifiwa kwamba kampuni ya Zain imetumbukiza zaidi ya $2.5 kwa ajili ya onyesho hilo kwani inasemekana kwamba kwa R.Kelly kukubali kufanya show yoyote nje ya Amerika Kaskazini basi $600,000 lazima ziwe mezani. Viingilio katika onyesho hilo ambalo tiketi zake zilishakwisha(sold out) wiki mbili zilizopita, vimepangwa kuwa Ushs 30,000(Silver) Ushs 125,000(Gold) na Ushs 250,000(Platinum). Hii ni mara ya kwanza kwa R.Kelly kufanya concert katika ukanda wa Afrika Mashariki. Na barani Afrika kwa ujumla mahali pengine ambapo amewahi kufanya onyesho ni Afrika Kusini tu.


R.Kelly ameahidi kuimba nyimbo zake zote ambazo amewahi kutamba nazo kama vile Bump n’Grind, I Believe I Can Fly,Gotham City,Ignition(Remix),The World’s Greatest,If I could turn back the hands of time, na nyinginezo tele bila kusahau hip-hopera yake ya Trapped In A Closet.

Sasa kwa wale ambao mmeshawahi kuhudhuria show yeyote ya R.Kelly,mnajua kwamba yeye hupenda mashabiki wanaokwenda naye sambamba.Hupenda kuwashirikisha hadhira(audience).Kazi kwenu.Jukwaani R.Kelly anatarajia kusindikizwa na wasanii wa Uganda Bebe Cool,Jose Chameleon,GNL,Peter Miles na Goodlyf ambao ni Radio na Weasel.Wote hao wamepigiwa kura na waganda wenyewe ili kupata nafasi hiyo. Pata uhondo zaidi PIGA CHABO BONGO CELEBRITY ILIKOTOKA TAARIFA HII

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...