Monday, January 11, 2010

Mchungaji Mtikila atupwa rumande



MWENYEKITI wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila atalazimika kukaa rumande kwa siku kadhaa baada ya hakimu kumfutia dhamana katika kesi yake ya kumkashifu Rais Jakaya Kikwete kutokana na kushindwa kufika mahakamani mara kadhaa.

Hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Waliarwande Lema alifikia uamuzi wa kumuweka rumande baada ya mchungaji huyo kushindwa tena kufika mahakamani na baadaye kudai kuwa alikuwa akimfuatilia daktari aliyemfanyia upasuaji baada ya kuumwa na nyoka.

"Sababu hizo, si za kutiliwa maanani na ili kutoendeleza tabia hiyo nakufutia dhamana," alisema Hakimu Lema baada ya kusikiliza utetezi wa Mtikila ambaye amewahi kugombea urais mara tatu kwa tiketi ya DP (Democtratic Party)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...