Wednesday, January 20, 2010
LILIAN MDUDA ATINGA FAINALI ZA "FACE OF AFRICA" LAGOS NIGERIA!!
Meneja Masoko wa Multchoice Tanzania Furaha Samalu akizungumza na waandishi wa habari kweye Hoteli ya SouthernSun jijini Dar es salaam leo wakati akitoa taarifa juu ya mshiriki wa Mnet Face of Africa Lilian Mduda ambaye yuko naye pichani kutoka Tanzania kutinga katika fainali za shindano hilo zitakazofanyika nchini Nigeria katika jiji la Lagos Februari 6/ 2010 ambapo washiriki 10 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliofanikiwa kuingia kwenye fainali hizo watachuana.
Tanzania ni moja ya nchi za Afrika ambazo zimekuwa zikipeleka wawakilishi mara kwa mara katika shindano hilo kubwa la uanamitindo katika bara la Afrika,
Kwa Tanzania mwanamitindo Miriam Odemba ndiye aliyewahi kushika nafasi za juu katika shindano hilo akiwakilisha Tanzania miaka ya nyuma na alifanikiwa kuingia mkataba wa kufanya kazi za uanamitindo na kampuni ya Elite Model Look ya Afrika Kusini.
Hata hivyo kampuni hiyo ilikatisha mkataba na Miriam Odemba na kumrejesha nyumbani baada ya mwanamitindo huyo kushindwa kufuata maelekezo ya kitaalamu aliyokuwa akipewa na wakuu wake katika kampuni hiyo ambapo inadaiwa alishindwa kufuata mpangilio mzuri wa kula chakula na mazoezi kitu kilichomfanya anenepe na kushindwa kukidhi viwango vya uanamitindo vilivyokuwa vikitakiwa na kampuni hiyo.
Mwakilishi wa mwaka huu Lilian Mduda ambaye ni mwanfunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam amesema amejiandaa vyema kwa ajili ya shindano hilo na haoni mshiriki yeyote anayemtisha isipokuwa ni yeye mwenyewe anayeweza kujiwekea mazingira ya kushinda kwa kuzingatia yale yote atakayoelekezwa na kuyafanya kwa ufanisi ili aweze kufikia malengo yake katika fainali hizo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
1 comment:
Good day, sun shines!
There have were times of hardship when I didn't know about opportunities of getting high yields on investments. I was a dump and downright stupid person.
I have never imagined that there weren't any need in big initial investment.
Nowadays, I feel good, I begin take up real income.
It gets down to choose a proper companion who uses your money in a right way - that is incorporate it in real deals, and shares the profit with me.
You may ask, if there are such firms? I'm obliged to answer the truth, YES, there are. Please get to know about one of them:
http://theinvestblog.com [url=http://theinvestblog.com]Online Investment Blog[/url]
Post a Comment