Sunday, January 31, 2010

Jerry Muro matatani



HARAKATI za Mwanahabari Bora wa Jumla wa Mwaka 2009 Tanzania, Jerry Muro, za kupambana na kero ya rushwa na ufisadi jana zilimwingiza mwandishi huyo mikononi mwa jeshi la Polisi akituhumiwa kuomba na kupokea rushwa.

Muro, ambaye alikuwa mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV na baadaye kuhamia kituo cha televisheni cha Taifa(TBC1), alikumbwa na mkasa huo leo majira ya saa sita mchana jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Sea Cliff.


Akizungumzia suala hilo Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema kuwa ni kweli mwandishi huyo amekamatwa na yuko polisi kwa mahojiano.

"Ni kweli yuko hapa na anahojiwa na mimi ndo ninapewa taarifa hivyo nitatoa taarifa kamili kesho saa sita,"alisema Kova.

"Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata, Muro alikamatwa kufuatia mtego uliowekwa na askari polisi mara baada ya kuarifiwa na mfanyabiashara mmoja (jina tunalihifadhi) ambaye ndiye aliyetakiwa kutoa fedha hizo."

Bila kufafanua kwa undani sababu za Muro kutaka kupewa fedha hizo, taarifa zinadai kuwa Muro alikamatwa muda mfupi baada ya kukabidhiwa fedha hizo

“Muro alikuwa ameahidiana na mfanyabiashara ...., ili ampe Sh10milioni kama hongo, lakini mfanyabiashara huyo alitoa taarifa kwa Polisi na ndio leo (jana) wamefanikiwa kumkamata. Walimkamata mara baada ya kupokea fedha hizo,” alisema mtoa taarifa.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...