TANZANIA NA CHINA ZATILIANA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO (MOU) UJENZI WA RELI YA KATI KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (aliyeipa mgongo kamera), akizungumza jambo kabla ya kutia saini Hati ya makubaliano ya ushirikiano wa ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati katika kiwango cha Kimataifa (Standard gauge) na Benki ya Exim ya China, Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (Kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamuriho (katikati) kabla ya kutia saini Hati ya makubaliano ya ushirikiano wa ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati katika kiwango cha Kimataifa (Standard gauge) na Benki ya Exim ya China, Jijini Dar es salaam Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (Kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja wa maafisa wa Benki ya Exim-China, kabla ya kutia saini Hati ya makubaliano ya ushirikiano wa ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati katika kiwango cha Kimataifa (Standard gauge), na Benki ya Exim ya China, Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na Naibu Meneja Mkuu (Mikopo Nafuu) wa Benki ya Exim ya China, Zhu Ying, wakitia saini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (Standard gauge), Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akipeana mkono na Naibu Meneja Mkuu (Mikopo Nafuu) wa Benki ya Exim ya China, Zhu Ying, mara baada ya kutia saini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (Standard gauge), Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (kushoto), akizungumza na Rais wa Benki ya Exim-China, Liu Liange, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya Rais huyo aliyekuwepo nchini kwa ziara ya kikazi kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (kulia), akipeana mkono na Rais wa Benki ya Exim-China, Liu Liange, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya Rais huyo aliyekuwepo nchini kwa ziara ya kikazi kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kuondoka nchini.
Rais wa Benki ya Exim kutoka China, Liu Liange (kulia) akiwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere, muda mfupi kabla ya kuondoka nchini kurejea China baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi nchini ambapo Benki yake imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kutekeleza Miradi Kadhaa ya Maendeleo ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa (Standard gauge)
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (kulia), akiagana na Rais wa Benki ya Exim-China, Liu Liange, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya Rais huyo aliyekuwepo nchini kwa ziara ya kikazi kwa mawaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Comments