MBUNGE WA UKONGA MWITA WAITARA ATEMBELEA SHULE NA KUKABIDHI MADAWATI NA VIFAA VYA MICHEZO
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Magole wakiwa wamebeba moja ya madawati waliokabidhiwa na Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara jana jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara, kulia akisalimiana na Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kiboga iliyopo Chanika Mvuti Dar es Salaam wakati alipoenda kukabidhi msaada wa madawati jana
Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara, akizungumza na kina mama wa kikundi cha Kikoba Cha Mpanga wa Vikoba kilichopo Magole wakati alipokuwa akitembelea jimbo hilo jana
Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya msingi Magole wakati alipokabidhi msaada wa madawati
Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara akimkabidhi msaada wa mipira Mwalimu wa Michezo, Emmanuel Zongo wa Shule ya Msingi Magole wakati alipokwenda kukabidhi msaada wa madawati jana
Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara akizungumza na na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbondole baada ya kukabidhi madawati jana
Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara, akiwafundisha somo la hesabu wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbondole baada ya kukabidhi madawati na vifaa vya michezo
Comments