DK. JOHN POMBE MAGUFULI ACHAGULIWA MWENYEKITI MPYA WA CCM, AMCHAGUA TENA KINANA KUWA KATIBU MKUU
Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete wakiwapungia mikono wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM baada ya wajumbe hao Kumthibitisha kuwa Mwenyekiti wa awamu ya Tano Kwa kumpigia kura zote za ndiyo wajumbe waliopiga kura ni 2395 kura zilizoharibika ni 0 na Mwenyekiti Dk. John Pombe Magufuli ameshinda kwa kwa kupigiwa kura zote 2395, Lakini pia mwenyekiti huyo ameamua kuendelea na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Sekretarieti nzima iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA)
Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipongezwa na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete mara baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa CCM.
Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akikabidhiwa ripoti ya uchaguzi uliopita na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisikiliza machache kutoka kwa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete kabla ya kukabidhiwa ripoti hiyo.
Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipokea ilani ya uchaguzi kutoka kwa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete.
Viongozi wastaafu wakiwa katika mkutano huo kutoka kushoto ni Mzee John Samwel Malecela, Mzee Amani Abeid Karum, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Mohamed Gharib Bilal na Mzee Pius Msekwa.
Mwenyekiti wa Chama cha TLP Ndugu Agustino Mrema akiwasliana na wake wa viongozi wastaafu.
Baadhi ya wajumbe wakishangilia mara baada ya mkutano huo kumthibitisha Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM.
Mwanachama wa CHADEMA Mgana Msindai akiwapungia mkono wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM baada ya kurejea CCM alipotangaza rasmi kwenye mkutano mkuu huo.
Mgana Msindai akielekea jukwaani ili kutangaza nia yake ya kurejea CCM leo kwenye mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma.
Freddy Mpendazoe aliyekuwa mwanachama wa chama cha CHADEMA akitangaza nia yake ya kurejea CCM kwenye mkutano mkuu wa Chama hicho uliofanyika mjini Dodoma leo.leo.
Comments