NHC ARUSHA YAZUNGUMZIA MAENDELEO YA UWEKEZAJI SAFARI CITY
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Arusha, James Kisarika akielezea mandhari ya mji wa kisasa wa SafariCity kwa waandishi wa habari.
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Arusha, James Kisarika na Ofisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Gibson Mwaigomole wakielezea ujenzi wa nyumba za mfano kwa waandishi wa habari kwenye eneo la Mradi wa Safari City katika eneo la ujenzi wa nyumba za mfano.
Ofisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Gibson Mwaigomole akifanya mahojiano na waandishi wa habari juu ya Mradi wa Safari City katika eneo la ujenzi wa nyumba za mfano.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakifuatilia taarifa ya mradi iliyokuwa ikitolewa na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Arusha, James Kisarika.
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeanza kuelekeza nguvu zake mkoani Arusha baada ya kutenga maeneo ya uwekezaji zaidi ya 600 kwa ajili ya uwekezaji na makazi.
Viwanja hivyo vipo eneo la Mateves mkoani Arusha na vitauzwa kwa wananchi.
Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Arusha, James Kisarika amesema mjini Arusha kuwa bei ya viwanja hivyo vitamwezesha mwananchi wa kawaida kumudu gharama.
Amesema katika mradi huo kutakuwapo na ujenzi wa nyumba mbalimbali za shughuli za kijamii ikiwamo shule, hospitali, kituo cha polisi, maeneo ya biashara na maendeleo ya viwanda vidogo vidogo.
Comments