MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM UNAENDELEA MJINI DODOMA
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dk. Jakaya Kikwete akiwahutubia wajumbe wa mkutano mkuu Maalum kwenye ukumbi wa Dodoma Convention Centre mjini Dodoma, ambapo mkutano huo utamthibitisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli aliyekaa kulia kuwa Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa akipokea uongozi huo kutoka kwa mtangulizi wake Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete, Wajumbe wengi wamehudhuria katika mkutano huo wanatarajia kupiga kura hiyo muda wowote kuanzia sasa
Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Bara , Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na wa pili kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa maelezombalimbali na kumkaribisha Mwenyekiti wa Chama Dk Jakaya Kikwete katika Mkutano Mkuu Maalum ili kuufungua tayari kwa kumthibitisha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti mtarajiwa wa CCM Dk. John Pombe magufuli wa pili kutoka kushoto akishiriki kuimba wimbo wa taifa pamoja na Mwenyekiti wa CCM anayeng’atuka madarakani Dk. Jakaya Kikwete wa pili kulia wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar wa tatu kutoka kushoto, Mwenyekiti Mstaafu wa CCM taifa Mzee Benjamin William Mkapa na kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Taifa Mzee Ali Hassan Mwinyi akishiriki kuimba nyimbo kabla wakati wa mkutano huo.
Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Hassan Suluhu, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar SMZ Mhe. Mohammed Said Mohammed Dimwa
Mama Salma Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu kutoka mkoa wa Lindi akishiriki kuimba nyimbo za hamasa na pamoja nawake wa viongozi wenzake.
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Part TLP Bw. Agustino Lyatonga mrema na viongozi wenzake wa vyama vilivyoalikwa katika mkutano mkuu Maalum wa CCM unaofanyika mjini Dodoma
Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Hassan Suluhu, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar SMZ Mhe. Mohammed Said Mohammed Dimwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakishiriki kuimba nyimbo za hamasa.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kushoto na Mzee Said El Maamry na wageni waalikwa wengine wakiwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndugu Anthony Dialo akiwa na wajumbe wenzake kutoka mkoani Mwanza wakiwa katika mkutano huo, Kulia ni Richard Ndasa na wa tatu ni Ndugu John Mongela.
Baadhi ya wajumbe kutoka mkoa wa Iringa kutoka kulia ni Dk Agustine Mahiga na Salim Abri Asas pamoja na wenzao wakiwa katika mkutano huo.Mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika mjini Dodoma
Mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika mjini Dodoma sasa hivi.
Baadhi ya wake wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo
Baadhi ya viongozi wastaafu wakipitia gazeti la uhuru lenye makala maalumu ya Dk. John Pombe Magufuli anayetarajiwa kuthibitishwa leo kuwa Mwenyekiti wa Cma cha Mapinduzi CCM.
Wajumbe kutoka Zanzibar wakiwa katika mkutano huo.
Wajumbe kutoka mkoa wa Morogoro nao hawakuwa nyuma kupitia makala ya Gazeti la Uhuru leo.
Mwimbaji wa kundi la Hamasa la CCM TOT Bi. Khadija Kopa na waimbaji wenzake wakitumbuiza katika mkutano huo.
Mmoja wa waalikwa akipata kumbukumbu katika mkutano huo.
Kundi la Hamasa la TOT likiendelea na burudani katika mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wakiongozwa na Mjumbe Angela Kairuki kutoka mkoa wa Dar es salaam wakiserebuka kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Dk. Fenella Mukangara kutoka mkoa wa Dar es salaam na Tambwe Munde kutoka mkoa wa tabora wakiserebeka pamoja na wajumbe wenzao.
Mjumbe Munde Tambwe akisalimiana na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Mzee Yusuf Makamba.
Mjumbe Fredrick Mwakalebela kutoka mkoa wa Iringa akiwa na wajumbe wenzake.
TOT ikiendelea kutumbuiza
Mwakipesile na Mary Mwanjelwa Wajumbe kutoka mkoani Mbeya wakisalimiana kwa furaha.
Comments