KOFFI OLOMIDE AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI 18 BAADA YA KUKUTWA NA HATIA YA KUMDHALILISHA DANSA WAKE


Koffi-Olomide-Arrest2Mwanamuziki wa Kimataifa wa Miondoko ya Dansi kutoka Nchini Congo, Antoine Christophe Agbepa Mumba maarufu kama “Koffi Olomide” amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela baada ya kuonekana na hatia ya kumdhalilisha kwa kumpiga dansa wake wakati wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nchini Kenya hivi karibini.
Mwanamuziki huyo alikamatwa mapema leo akiwa nyumbani kwake katika mji wa Kinshasa na kupelekwa Mahakamani moja kwa moja na kukutwa na hatia hiyo.
Hukumu hiyo imetolewa baada ya ushahidi huo kuonekana akimpiga dansa wake na atatakiwa kuitumikia adhabu hiyo kwani hajapewa nafasi ya kulipa faini ya aina yoyote ile.
hatua ya kumkamata Mwanamuziki huyo ilifikiwa baada ya kuanzishwa kwa kampeni ya baadhi ya wadau wa maswala ya kijamii wakiongozwa na Zakarie Bababaswe aliyefungua kesi kwa niaba ya Serikali ikiwa ni madai ya udhalilishaji kwa dansa wake, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kongo, kuamua kukamatwa kwake na kusema anataka haki itendeke.

Comments

Popular posts from this blog

JESHI LA MAGEREZA NCHINI WAJADILIANA NA NHC NAMNA YA KUENDELEZA MAKAZI MAKAO MAKUU DODOMA

Baraza Jipya la Mawaziri