BALOZI OMBENI SEFUE ATEMBELEA TAASISI YA WAKALA WA TAIFA WA UTAFITI WA NYUMBA BORA NA VIFAA VYA UJENZI (NHBRA)

1Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi na Vifaa vya Ujenzi  (NHBRA) wakati alipofanya ziara katika taasisi hiyo mwishoni mwa wiki ili kujionea shughuli  mbali mbali zinazofanywa na taasisi hiyo ,  Kwa kiwango kikubwa (NHBRA)  imeonyesha ni taasisi inayoweza kujenga nyumba za bei nafuu sana hasa vijijini ili watanzania wa maeneo hayo waweze kupata makazi bora ya kuishi kwa bei  rahisi zaidi, Kulia katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Bw.Matiko Samson Mturi.
Taasisi hiyo pia imekuwa ikijihusisha na  mafunzo teknolojia ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa  vikundi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kuwafundisha juu ya utengenezaji wa matofali, vigae vya kuezekea nyumba pamoja na ujenzi wa nyumba za zenyewe ambapo  taasisi na wananchi mbalimbali wanaweza kufaidika na mpango huo nchini.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)2Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Bw.Matiko Samson Mturi akizungmza wakati alipokuwa akimkaribisha Balozi Ombeni Sefue wakati alipotembelea katika taasisi ya Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi  NHBRA Mwenge jijini Dar es salaam.
3Bw. Sylivester Shumbusho Fundi kutoka Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi  NHBRA akimpa maelezo Balozi Ombeni Sefue juu ya utengenezaji wa matofali ya bei rahisi kwa kutumia udongo wakati alipokuwa akitembelea karakana ya taasisi hiyo iliyopo Mwenge jijini Dar es salaamKatikati ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiko Samson Mturi.
4Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiko Samson Mturi akimpa maelezo Balozi Ombeni Sefue wakati alipokuwa akitembelea na kukagua shughuli mbalimbali katika taasisi hiyo kulia ni Bw. Sylvester Shumbusho Fundi katika taasisi hiyo.
6
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na shughuli za kutengeneza vigae vya kuezekea nyumba katika karakana ya taasisi hiyo.
7
Balozi Ombeni Sefue akitembezwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiku Samson Mturi maeneo mbalimbali  ili kujionea shughuli za  zinazofanywa na taasisi hiyo.
8Balozi Ombeni Sefua akishiriki katika shughuli ya kufyatua matofali kazi inayofanywa pia na Taasisi hiyo kwa kutoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali nchini kote.
9Balozi Ombeni Sefua akiangalia kazi  ya kufyatua matofali  inayofanywa pia na Taasisi hiyo kwa kutoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali nchini kote.
10
Balozi Ombeni Sefue akiangalia wafanyakazi wa taasisi hiyo wakati wakitengeneza vigae kwa ajili ya kuezekea nyumba.
11
Balozi Ombeni Sefue akipiga picha kwa simu yake huku wafanyakazi wa taasisi hiyo wakimuangalia baada ya moja ya nyumba ndogo iliyojengwa katika ghala ya taasisi hiyo kwa ajili ya mfano kumfurahisha.
12Balozi Ombeni Sefue pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiko Samson Mturi wakipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo mara baada ya kukamilika kwa ziara hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

JESHI LA MAGEREZA NCHINI WAJADILIANA NA NHC NAMNA YA KUENDELEZA MAKAZI MAKAO MAKUU DODOMA

Baraza Jipya la Mawaziri