BODI YA NHIF YAUNDA MUUNDO MPYA WA WAKURUGENZI KUTOKA WAKURUGENZI TISA HADI WATANO
Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Spika Mstaafu, Anne Makinda akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya maboresho ya muundo wa safu ya wakurugenzi leo jijini, Dar es Salaa,Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernald Konga.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernald Konga akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua ya bodi waliochukua katika shirika hilo katika kubadili muundo wa wakurugenzi, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF Spika Mstaafu, Anne Makinda.
Wajumbe wa bodi na waandishi habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Spika Mstaafu, Anne Makinda. Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii
Na Chalila Kibuda, Blogu ya Jamii
BODI ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imefanya maboresho kwa kupunguza idadi ya wakurugenzi kutoka tisa hadi watano ili kuweza kufanya kazi kwa kasi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Na Chalila Kibuda, Blogu ya Jamii
BODI ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imefanya maboresho kwa kupunguza idadi ya wakurugenzi kutoka tisa hadi watano ili kuweza kufanya kazi kwa kasi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi habari Makao Makuu NHIF leo Mwenyekiti bodi hiyo Spika Mstaafu, Anne Makinda amesema kuwa utaratibu wa awali wakurugenzi walikuwa wanaajiliwa kwa mikataba ya miaka mitatu mitatu.
Amesema kuwa wakurugenzi waliokuwa wanafanya kazi ambapo wengine kwa mikataba na wengine wamemaliza na ambao walikuwa wanaendelea wamesitisha mikataba yao.
Makinda amesema kuwa NHIF imekaa kwa muda ikiwa haina bodi kwa mwaka mmoja na nusu hivyo baadhi ya vitu havikuwa sawa.
Amesema kuwa watu ambao wamemaliza mikataba na weengine kusitisha mikataba yao wanaweza wakaomba tena kama wana sifa ya kazi watazoomba na kuangalia weledi wao
Comments