MARUFUKU RUSHWA KATIKA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI

B1Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akipekua mafaili ya hukumu za migogoro ya ardhi ili kujiridhisha kama haki inatendeka kwa wananchi wakati alipotembelea Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini.
B2Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini.
B3Baadhi ya watendaji na watumishi wa umma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula katika ofisi za Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini.
…………………………………………………………………………………………………
Na Hassan I. Mabuye
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula ayataka Mabaraza ya Ardhi na Nyumba kuepuka rushwa kutoka kwa wenye fedha ili kuwapa upendeleo na kukandamiza wanyonge katika maamuzi yahusuyo migogoro ya ardhi. Mheshimiwa Mabula ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Naibu Waziri amepiga marufuku tabia ya baadhi ya watu ambao huwapa pesa waendesha mashtaka na wenyeviti wa mabaraza ya Ardhi na nyumba ili kupindisha sheria.

Comments

Popular posts from this blog

JESHI LA MAGEREZA NCHINI WAJADILIANA NA NHC NAMNA YA KUENDELEZA MAKAZI MAKAO MAKUU DODOMA

Baraza Jipya la Mawaziri