MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WATAKIWA KUWA TAYARI KUFANYA KAZI VIJIJINI
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Enterberth Nyoni akitoa ufafanuzi kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kuhusu uboreshaji wa vyuo kwa kujitegemea wakati wa kikao kazi cha wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii mjini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii waliohudhuria Kikao Kazi mjini Dodoma wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kikao hicho leo mjini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw.Dickson Rusage akitoa ufafanuzi kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kuhusu matumizi mazuri ya rasilimali fedha, watu, utunzaji wa mali za Serikali na Utekelezaji wa dhana ya Utawala Bora katika Taasisi za Maendeleo ya Jamii leo mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Eliasifu Mlay akitoa ufafanuzi kuhusu uzingatiaji wa Maadili katika Utumishi wa Umma wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii leo mjini Dodoma.
Na.Aron Msigwa - Dodoma.
Maafisa Maendeleo ya Jamii wanaohitimu mafunzo katika vyuo mbalimbali nchini na wale waliko kazini wametakiwa kuwa tayari kufanya kazi vijijini ili kuwawezesha wananchi kuzitumia fursa za maendeleo zilizoko katika maeneo wanayoishi kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Enterberth Nyoni wakati akitoa ufafanuzi kuhusu Utendaji Kazi wa Maafisa hao wakati wa kikao kazi cha wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii mjini Dodoma.
Amesema Maafisa Maendeleo popote walipo lazima watambue kuwa wao ni dira na chachu ya mabadiliko ya kuwafanya wananchi kubadilika kwa kufanya kazi kulingana na mabadiliko na rasilimali zilizopo katika maeneo yao.
Comments