KAMPUNI YA KANJI LALJI YATOZWA FAINI


Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh, Luhaga Mpina akipata maelezo kutoka kwa mbunge wa temeke mh,Abdallah Mtolea kuhusu uchafuzi wa mazingira wilaya ya temeke mapema hii leo 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh,Luhaga Mpina akipata maelezo kutoka kwa uongozi wa kiwanda cha bia serengeti alipofanya ziara ya kukagua Mazingira katika eneo hilo la viwanda linalotuhumiwa kuchafua mazingira. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupiga faini viwanda vitatu ambavyo vimetuhumiwa kuchafua mazingira wilaya ya temeke mtaa wa serengeti. 

Kampuni ya usafirishaji ya Kanji Lalji iliyopo mtaa wa Serengeti wilayani Temeke jijini Dar es Salaam imetozwa faini ya shilingi milioni ishirini na laki tano, na kutakiwa kulipa faini hiyo ndani ya siku saba, kwa kosa la kutiririsha maji yenye sumu katika mitaro ya maji ya mvua inayoelekea kwenye makazi ya watu na mazingira na hivyo kuhatarisha maisha na afya za viumbe hai.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ametoa kauli hiyo leo kupitia Baraza la Taifa na Hifadhi ya Mazingira NEMC katika ziara yake ya kukagua viwanda na usafi wa mazingira jijini dar es salaam.

Ziara hiyo ya Naibu waziri Mpina, iliyopelekea naibu waziri huyo kuinuka Ofisini na kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika baadhi ya viwanda hivyo, imetokana na malalamiko ya baadhi ya wanachi katika maeneo husika hususan wenye viwanda.

Naibu waziri mpina amesema kuwa kutozwa faini ni hatua ya pili kwa baadhi ya viwanda baada ya kupewa onyo na maelekezo na NEMC na manispaa, na aliongeza kuwa kwa kutokutii taasisi za serikali baada ya adhabu hii hatua itakayofuata ni ya kuvifungia viwanda hivyo.

Kwa upande mwingine Mhe. Mpina amekipongeza kiwanda cha Serengeti breweries kwa kutii kauli ya serikali kwa kulipa faini iliyotozwa awali ya kiasi cha shilingi milioni kumi na sita kwa kosa la uchafuzi wa mazingira na kuwashukuru wakazi wanaozunguka kiwanda cha SBL pamoja na Mbunge wa TEMEME (CUF) Mhe.Abdallah Mtolea kwa kutoa taarifa za uchafuzi wa mazingira na kukipa kiwanda hicho siku 45 kufanya marekebisho madogo madogo ya kimazingira kiwandani hapo.

Aidha, Adhabu nyingine ya uharibifu na uchafuzi wa mazingira imetolewa kwa wamiliki wa eneo la kampuni ya CI group, ambao ni Prime Liberty Limited ya kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 15 kwa muda wa siku saba, na kufanya jumla ya faini za uchafuzi wa mazingira zilizotozwa kwa siku ya leo kuwa shilingi milioni 39 na laki tano.

Comments

Popular posts from this blog

JESHI LA MAGEREZA NCHINI WAJADILIANA NA NHC NAMNA YA KUENDELEZA MAKAZI MAKAO MAKUU DODOMA

Baraza Jipya la Mawaziri