Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita Barabarani kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako pamoja na mambo mengine kesho tarehe 23 Januari, anatarajiwa kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la 57/15.
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani Monduli.
Baadhi ya Wananchi wa Maeneo ya Sanawali wakishangilia ujio wa Rais John Pombe Joseph Magufuli,alipokuwa akielekea Wilayani Monduli mapema leo asubuhi.
Rais Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu wananchi katika maeneo ya SANAWARI, TEKNIKO, NGARENARO, MBAUDA, MAJENGO na KISONGO
No comments:
Post a Comment