Tuesday, January 12, 2016

WAZIRI KITWANGA AKUTANA NA VIONGOZI WA WILAYA YA MISUNGWI, ACHANGIA MIRADI YA MAENDELEO

MIS1

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza mara baada ya kupokelewa wilayani hapo. Waziri Kitwanga aliwataka viongozi hao kuongeza nguvu kubwa ya kukusanya kodi kwa wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa na si kuwasumbua wafanyabiashara wadogowadogo. Pia aliwataka viongozi hao wahakikishe hakuna mwanafunzi atakayekaa chini darasani ifikapo mwakani. Picha zote na Felix Mwagara.
MIS2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akiwauliza maswali viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakati alipokuwa anakagua ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari Aimee Milembe wilayani humo.
MIS3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akiwauliza maswali viongozi wa Kata ya Mabuki wilayani Misungwi wakati alipokuwa anakagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mhungwe katika kata hiyo. Waziri Kitwanga alichanga milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Kituo hicho cha afya. Wapili kulia ni Diwani wa Kata hiyo, Nicodemus Ihano, na wapili kushoto ni Mtendaji wa Kata hiyo, Angelina Nyanda..
MIS4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kushoto) akiangalia ufa katika moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Lubuga iliyopo Kata ya Mabuki wilayani Misungwi. Waziri Kitwanga aliagiza darasa hilo livunjwe na ameahidi kuchangia matofali pamoja na mifuko ya saruji…
MIS5
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akimsalimia Diwani wa Kata ya Misungwi, Mwamba Makune, wakati Waziri huyo alipokuwa anawasili katika Shule ya Sekondari ya Aimee Milembe jimboni humo kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na viongozi wa Serikali ya vijiji katika Kata ya Misungwi.
MIS6
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mwajuma Nyiruka akizungumza na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) ili azungumze na wakuu hao wa idara. Waziri Kitwanga aliwataka viongozi hao waongeze nguvu ya kukusanya kodi kwa wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa na si kuwasumbua wafanyabiashara wadogowadogo. Pia aliwataka viongozi hao wahakikishe hakuna mwanafunzi atakayekaa chini darasani jimboni humo ifikapo mwakani. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Nathan Mshana. Picha zote na Felix Mwagara.

No comments:

Rais wa Sierra Leone Awasili nchini

Rais wa Jamhuri ya Sierra Leone, Mheshimiwa Julius Maada Bio, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kilele wa Wak...