Sunday, January 24, 2016

NAIBU KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

VIT1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Mwaimu (kulia), wakati alipotembelea kituo cha kumbukumbu cha Mamlaka hiyo, mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam. Kushotoni Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho (NIDA), Paul Bwathondi.
VIT2
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Mwaimu (kushoto),akimuongoza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya NdaniyaNchi, Balozi Simba Yahya (kulia),kutembelea ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, mwishonimwa wiki ,jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kuona jinsi shughuli zaUchapaji na Uzalishaji wa Vitambulisho vya Utaifa zinavyofanyika.
VIT3
Msimamizi wa Mifumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Ami Mohamed (kulia), akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), jinsi taswira ya muombaji kitambulisho inavyohifadhiwa kwenye mfumo ili kuwezesha kuiweka kwenye kitambulisho. Naibu Katibu Mkuu  alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
VIT4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia),akiuliza swali baada ya kupata maelezo kutoka kwa Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Noel Chikwindo (kushoto), Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
VIT5
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (aliyenyooshamkono), akifuatilia kwaumakini uhakiki wa taarifa za muombaji wa Kitambulisho cha Utaifa, wakati alipotembelea kitengo cha Uhakiki waTaarifa cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi .Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
VIT6
Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Paul Bwathondi (kulia), akitoa ufafanuzi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (watatu kutoka kulia waliosimama), Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
VIT7
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia), akielezea jambo wakati alipotembelea Kitengo cha kudhibiti ubora wa Vitambulisho vya Taifa, kilichopo kwenye Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),Katikati ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi na kushoto ni Afisa Usajili anayeshughulikia ubora, Jemima Mulokozi. Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
VIT8
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), anayeshughulikia ubora, Jemima Mulokozi (kushoto), akimuelezea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), jinsi wanavyothibiti ubora wa Kitambulisho cha Utaifa kabla akijachapishwa.Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.( (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...