Wednesday, January 13, 2016

SERIKALI YAMPA ZAWADI YA KIWANJA NA FEDHA MBWANA SAMATTA

mbv2
Mchezaji Mbwana Samatta aliyejishindia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa Ndani nchini Nigeria akimkabidhi jezi yake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makzi Mh. Wiliam Lukuvi katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jiji Dar es salaam usiku huu.
mbv3
Baadhi ya wanamichezo waliohudhuria katika hafla hiyo kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajiri ya Simba Bw. Zakaria Hanspope, Saleh ali Mhariri wa Gazeti la michezo la Champion na Wakili wa Vilabu shiriki vya Ligi kuu Tanzania Bara mwanasheria Damas Ndumbalo wakibadilisha na mawazo katika hafla hiyo
2e109983-c68f-4a79-867d-c15254d9c956
Mchezaji Mbwana Samatta aliyejishindia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa Ndani nchini Nigeria amezawadiwa na serikali kiwanja kilichpo Kigamboni jijini Dar es salaam na fedha taslimu ambazo kiasi chake hakijafahamika hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makzi Mh. Wiliam Lukuvi anayeonekana katika picha  katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa wa serikali.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria katika hafla hiyo ni Waziri wa Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na viongozi wengine wengi wa serikali na wanamichezo.
Mbwana Samatta aliyekuwa akicheza mpira wa kulipwa katika timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inayomilikiwa na tajiri wa madini  na aliyewahi kuwa Gavana wa jimbo la Katanga nchini humo Moise Katumbi anatarajiwa kujiunga na timu ya  KRC Genki ya Belgium barani ulaya,  Hafla hiyo imefanyika usiku huu jijini Dar es salaam.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...